22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Baby Madaha: Naanzaje kuwa na mwanaume mdogo  

Baby MadahaNA BEATRICE KAIZA

MWIGIZAJI wa filamu za Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’, ameibuka na kudai kwamba anashangazwa na waigizaji wa kike waliopo katika mapenzi na wanaume wa umri mdogo.

Baby Madaha ambaye ameolewa na Mwarabu wa Dubai, amesema tabia ya wasanii wenzake kuwa na wanaume wenye umri mdogo maarufu ‘Serengeti Boys’ unafedhehesha na haiwasaidii chochote zaidi ya kujishushia hadhi yao.

Baby Madaha aliongeza kufafanua kwamba, tabia iliyojengeka kama fasheni kwa wasanii wakike watu wazima kuwa na wanaume wenye umri mdogo bila aibu wala kujifikiria athari zake ikiwemo kujishushia hadhi zao.

“Sijawahi kuwaza kama nitakuwa na Serengeti boy kwangu hawana nafasi sioni faida yoyote kwao, mimi nawashangaa kwa kuwa wengi wao wanatafuta umaarufu hakuna mapenzi wala maisha endelevu hapo,” alifafanua Baby Madaha

Hata hivyo, Baby Madaha, aliongeza ushauri wake kwa kuwataka wasanii wenzake kuwa na wanaume wenye umri wao ama wawe na wanaume watu wazima kama wanataka kulinda heshima zao na kujiongezea mashabiki badala ya kuwa na wanaume wenye umri mdogo.

Baadhi ya wanawake wasanii walio katika uhusiano wa kimapenzi na wanaume wenye umri mdogo ni pamoja na Wema Sepetu (28) na Idrissa (22), Zari (36) na Diamond (27), Aunty Ezekiel (30) na Iyobo, Jaquline Wolper (29) na Harmonize.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles