30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

TMDA yazindua mradi wa kudhibiti majaribio ya dawa kwa binadamu

Na Aveline Kitomary

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imezindua mradi unaolenga kudhibiti mifumo ya majaribio ya dawa kwa binadamu na tafiti mbali mbali zinazofanyika.

Akizungumza leo Novemba 26, baada ya kuzindua mradi huo wa miaka miwili na nusu Mganga Mkuu wa Serikali Prof Abel Makubi amesema mradi huo utawasaidia kuhakikisha majaribio ya dawa kwa binadamu nchini inakuwa kwa viwango stahili.

“Mkatoe majibu yanayotarajiwa,kama ni dawa ikaonekane inauwezo wa kutibu binadamu,kama kipimo ikaonyeshe kuwa na uwezo wa kugundua maradhi,mradi huu ukawe chachu kwa TMDA kuondoa baadhi ya changamoto katika shughuli zake,ikiwemo kuchelewa kutolewa majibu haraka za majaribio ya dawa zinazofanyika nchini”amesema.

Prof Makubi amesema kuna haja ya TMDA kuangalia gharama zinazotozwa hasa kwa wanafunzi wanaofanya majaribio ya dawa ikiwa ni sehemu ya masomo yao kwani wamekuwa wakipitia changanmoto nyingi kumudu gharama zilizopo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Adam Fimbo alisema utekelezaji wa mradi huo, utawasaidia kwa kiwango kikubwa kuboresha mifumo ya dawa,namna ya kupitisha maombi ya dawa kabla ya kufanyika nchini na kuweka mifumo bora itakayofuatilia watumiaji wa dawa za majaribio.

“Tutaweka mfumo ambao utahakikisha wote wanaotumia dawa za majaribio wanakuwa salama muda wote na kuwatunza wote wanaoshiriki katika majaribio ya dawa,” amesema .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles