27.4 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Madiwani Kiteto wapendekeza majina ya mwenyekiti na makamu

Na MOHAMED HAMAD, KITETO

MADIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kiteto katika Mkoa wa Manyara, wamependekeza majina ya mwenyekiti na makamu wake kuongoza halmashauri.

Mapendekezo hayo yatawasilishwa kikao cha madiwani ambapo hata hivyo watakaowapitisha ni madiwani wa CCM kwa kutokuwa na vyama vya upinzani.

Aliyeshinda uchaguzi huo ni Diwani wa Kata ya Songambele Abdallah Bundallah, aliyepata kura 20 kati ya 13 alizopata Lairumbe Mollel aliyekuwa mwenyekiti awali.

Makamu wa mwenyekiti aliyechaguliwa ni Kassimu Msonde CCM kata ya Kibaya kwa kura 20 dhidi ya Ramadhami mpolonge CCM kata ya Njoro kwa kura 12.

Mwenyekiti wa CCM Kiteto, Mohamed Kiyondo alisema uchaguzi umefanyika bila kuwepo na dalili za rushwa na waliochaguliwa ni takwa la wajumbe hao.

Baadhi ya wajumbe walisema wametenda haki kuwapata viongozi hao kwa kuwa wamezingatia uwakilishi wa makundi yote wilayani Kiteto hasa wakukima na wafugaji.

“Mbunge aliyepatikana ametokana na jamii ya kifugaji, sasa mwenyekiti ilikuwa lazima apatikane kutoka kwa wakulima kama kundi kubwa ili kuweka usawa ngazi ya uongozi,”alisema mmoja wa madiwani ambaye hakutaka kutaja majina yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles