25.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Wagika, Wagalu kunogesha tamasha la Simiyu Jambo Festival

Na Derick Milton, Simiyu.

Mashindano ya Ngoma za asili kutoka tabaka mbili za kabila la wasukuma katika Mkoa wa Simiyu (Wagika na Wagalu), zinatarajia kufanyika katika Tamasha kubwa la michezo mkoani humo (Simiyu Jambo Festival).

Mbali na Mashindano hayo ya ngoma, Tamasha hilo linatarajia kushirikisha zaidi ya wanamichezo 300 wa mbio za baiskeli pamoja na riadha kutoka mikoa mbalimbali nchini ambapo litafanyika jumamosi ya wiki hii mjini Bariadi.

Akiongea na waandishi wa habari leo Alhamis Novemba 26, Mratibu wa tamasha hilo Zena Mchujuko, amesema kuwa mbio za baiskeli washirikia watakimbia umbali wa kilometa 140 kwa wanaume na wanawake kilometa 80, na watu wenye ulemavu ambao watakimbia kilometa 5.

“ Tutakuwa na mashindani ya Insha kwa wanafunzi wa shule za sekondari mkoani mzima, lengo la Tamasha hili ni kutangaza utamaduni wa mkoa wetu, lakini kutakuwepo na mbio fupi za riadha kilometa 10 kwa wanaume na wanawake.

“ Tunajua utamaduni wa wasukuma kwa muda wote umekuwa kwenye ngoma za asili ambazo ni wagika na wagalu, lakini pia mchezo wa kukimbiza baiskeli umekuwa maharufu huku, pamoja na riadha,” ameongeza Mchujuko.

Ofisa Miradi kutoka Shirika la kimataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani (UNFPA) ambao ndiyo wadhamini wakuu wa Tamasha hilo Denis Swai alisema kuwa kauli mbiu ya Tamasha hilo mwaka huu ni “ Wezesha wanawake na wasichana kwa maendeleo ya Dunia,”

Katibu tawala wa Mkoa huo Miriam Mmbanga aliwataka wananchi wa mkoa huo pamoja na wafanyabishara kujitokeza kwa wingi wakati wa tamasha hilo kwa ajili ya kutangaza biashara zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles