30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaionya TFF, kisa Ligi Kuu Bara

Zainab Iddy, Dar es Salaam

BAADA ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kutangaza ligi zitachezwa bila mashabiki kutokana na tishio la virusi vya Corona, Serikali kupitia Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yusuph Singo, amelitaka shirikisho hilo kutokurupuka na badala yake kufuata maagizo yatakayotolewa na mamlaka husika.

Hivi karibuni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alitangaza kusitisha shughuli zote zinazoleta mkusanyiko ikiwamo michezo kwa siku 30 kuanzia Machi 18, mwaka huu, ili kupunguza ongezeko la janga la Corona nchini.

Akizungumza na MTANZANIA juzi, Singo alisema wizara ilisikia kile kilichozungumzwa na TFF, lakini walifanya haraka kutoa uamuzi kabla ya kujua kipi ambacho serikali itasema baada ya siku 30 kumalizika.

“Baada ya siku 30 zilizotolewa na Serikali kumalizika, wizara husika itakuja na taarifa ambayo ndivyo itakayotoa mwongozo kulingana na hali ya ugonjwa wa Corona itakavyokuwa kipindi hicho.

“Inaweza ligi kuendelea au kutoendelea, kama itaendelea vipi itafanyika, wizara ndiyo itakayozishauri mamlaka husika, kilichozungumzwa na TFF ni mapema mno,” alisema.

Singo aliongeza: “Zuio la siku 30 limeigusa michezo mingi kwani katika soka mbali na ligi kulikuwa na timu za taifa, lakini pia bado kuna michezo iliyokuwa ikijiandaa na Olimpiki na mashindano mengine mengi yote hiyo itapewa mwongozo jinsi gani watakavyoendelea na shughuli zao kama itabidi kuwa hivyo.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles