27.6 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Bashiru awaweka pabaya wakuu wa mikoa inayozalisha pamba

Derick Milton -Simiyu

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Dk. Bashiru Ally, amesema kuwa wapo baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya kwenye mikoa inayozalisha pamba nchini  wanaweza kuondolewa kwenye nafasi hizo ikiwa watashindwa kutimiza wajibu wao katika kuhakikisha pamba iliyoko kwa wakulima inanunuliwa.

Amesema ikiwa viongozi hao watashindwa kutoa taarifa kila saa na kila siku kwa viongozi wa chama hicho wilaya, mikoa na taifa  kuhusu hali ya ununuzi wa zao hilo basi watafukuzwa kazi maana watakuwa wameshindwa kutimiza wajibu wao.

Kauli hiyo aliitoa jana wilayani Maswa mkoani Simiyu, katika ziara yake ya siku moja ya kukagua hali ya ununuzi wa pamba kwa wakulima.

“Kuna wakuu wa wilaya na mikoa ambayo inazalisha pamba wanaweza kupoteza kazi kutokana na jambo hili la pamba ikiwa watashindwa kutimiza wajibu wao na wakulima wetu wakapata haki yao.

“Na kwa wakati, lazima kila saa, kila siku, na kila wiki mtoe taarifa juu ya ununuzi ulivyo, CCM tunataka hadi kufika mwishoni mwa mwezi huu yote iwe imenunuliwa na wakulima wamepata pesa zao,” alisema Dk. Bashiru.

Akiwa katika mji wa Malampaka Katibu Mkuu huyo  alishangaa kukuta pamba nyingi ikiwa imehifadhiwa kwenye ghala la Chama cha Msingi cha Ushirika Malampaka ikiwa bado hajanunuliwa huku wakulima wakiwa nje ambapo alieleza namna wanavyosotea soko huku mnunuzi akiwa ameshindwa kuwalipa kama serikali ilivyotoa maelekezo.

“Wakuu wa mikoa msicheke, tuko katika vita kubwa ya uchumi, hili ambalo nimeliona hapa malampaka, nisingelipenda kuliona sehemu nyingine tena, sitaondoka Mkoa wa Simiyu ikiwa nitaona suala la pamba linasuasua, tunataka kuona pamba yote inanunuliwa, benki tayari zimetoa pesa na wengine wanaendelea kununua,” alisema Dk. Bashiru.

Katibu Mkuu huyo wa CCM alisema katu chama chao hakitakubali kuona wakulima wa pamba wanaendelea kuteseka na zao hilo kwa kushindwa kununuliwa huku serikali ikiwa tayari imefanya jitihada za kuhakikisha wanunuzi wanapata pesa na kuanza kununua.

“Kama mkuu wa wilaya upo na mkulima anaendelea kunyanyasika, pamba yake inanunuliwa chini ya bei elekezi ya Shilingi  1200, wakati una polisi na vyombo vya usalama, tutakuondoa, hufai kuwepo katika nafasi hiyo, CCM hatutakubali wakulima wetu wanyanyasike hivyo,” alisema 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles