22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama Kuu yafuta maombi ya Askofu Kameka

Kulwa Mzee, Dar es salaam

MAOMBI ya Askofu Mulilege Kameka anayeshikiliwa mahabusu gerezani kwa zaidi ya miezi tisa sasa kwa madai si  raia wa Tanzania ya kutaka Mahakama Kuu iwatie hatiani Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kamishna wa Uhamiaji yamefutwa.

Maombi hayo yalifutwa jana Mahakama Kuu  Kanda ya DAR es Salaam mbele ya Jaji Atuganile Ngwala, aliyesikiliza pingamizi lililowasilishwa na wajibu maombi wakiyapinga kusikilizwa na mahakama hiyo.

Askofu Kameka  ni Askofu wa Kanisa la House of Prayer Shield of Faith Christian Fellowship (HPSFCFC) aliwasilisha maombi hayo ambayo pia anaitaka mahakama hiyo iwahukumu kifungo Mwanasheria  Mkuu wa Serikali na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji kwa kudharau amri ya mahakama iliyoelekezwa kuachiwa huru ndani ya siku mbili.

Machi 18, mwaka huu, mahakama hiyo iliamuru askofu huyo aliyekuwa anayeshikiliwa akidaiwa kuwa sio raia wa Tanzania aachiwe huru kwani uraia wake hauna mashaka na kama kuna pingamizi litolewe ndani ya saa 48.

Amri hiyo ilitolewa na Jaji IIvin Mgeta, ambaye alitoa maelekezo kuwa askofu huyo atolewe mahali anaposhikili kwani vilelezo vilivyotolewa vimedhibitisha uraia wake kuwa ni Mtanzania.

Akitoa uamuzi Jaji Ngwala alisema hakuna Mahakama wala mabaraza yanayoweza kusikiliza maombi ambayo hayakufata utaratibu wakati wa kuwailishwa.

Alisema taratibu zinatakiwa kufuatwa na anakubaliana na hoja za wajibu maombi kwamba kifungu kilichotumika kuwasilisha maombi hayo, kifungu namba 392(a) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 na kifungu namba 114 hakiko sahihi.

Alisema anakubali kwamba mwombaji alitakiwa kushtaki kwa kutumia kifungu cha Sheria ya Makosa ya Jinai namba 9.

“Kwa sababu hizi pingamizi lililowasilishwa na wajibu maombi nalikubali, hoja za msingi, maombi nayafuta kwa sababu hayajaletwa kisheria, hayako kama yanavyotakiwa kuwa kisheria,” alisema Jaji.

Wakili wa mwombaji, John Mallya alisema kufutwa kwa maombi hayo ndio mwanzo wa safari kwani wanaweza kufungua kesi ya madai au kesi ya jinai  Jumanne wiki ijayo itategemeao watakayokubaliana na mteja wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles