30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Korosho zadaiwa kuchochea migogoro ya ardhi

Hadija Omary, Lindi

Imeelezwa kuwa kukua kwa shughuli za kiuchumi hasa kukua kwa kilimo cha korosho Wilaya ya Lindi mkoani hapa,  kumechochea kuongezeka kwa mashauri ya  ardhi kutoka 50 mwaka 2016 hadi kufikia 160 mwaka jana.

Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi mkoani hapa, Saidi Wambili amesema hayo jana akizungumza na Mtanzania Digital wakati wa kilele cha Siku ya Sheria nchini zilizofanyika katika Viwanja vya Ilulu Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.

“Ongezeko hilo la mashauri limekuwa kubwa kutokana na shughuli nyingi za kiuchumi zinazoendelea katika wilaya hiyo hasa za uanzishwaji wa mashamba ya korosho.

“Zao la korosho nadhani kwamba halina ubishi kwamba yeyote anayelima korosho maana yake anazungumzia fedha na anaipata kwenye korosho kwa hivyo jambo hilo limesababisha kuibuka kwa migogoro mingi ya ardhi ndani ya Wilaya ya Lindi,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa za kipindi cha miaka mitatu, baraza hilo husikiliza na kutoa hukumu kwa mashauri yasiyopungua 20 hadi 30 kwa mwezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles