27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Simai: Tamasha la Sauti za Busara ni kichocheo cha uchumi wa nchi

Festo Polea, Zanzibar

Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotions, Simai Mohammed, amesema tamasha la Kimataifa la Muziki la Sauti za Busara ni kichocheo cha uchumi wa Zanzibar kupitia utalii kwa ujumla.

“Kuanzia leo tutashudia burudani ya muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali wa ndani na nje, wanamuziki hao wataonyesha nyimbo za tamaduni za nchi zao zenye mafunzo, burudani na jumbe mbalimbali kwa watu wote.


Muziki ni biashara, muziki ni kazi na ni kazi kubwa hivyo inapaswa wananchi wajitokeze kwa wingi kushuhudia tamasha hilo.” Ameeleza Simai.

Aidha, Simai amesema viongozi wa Busara Promotions ambao ni waasisi na waandaaji wa tamasha hilo, wamekuwa wakifanya kila aina ya mbinu kuhakikisha tamasha hilo linakuwa na ubora wake hivyo amewasa wananchi Wazanzibar kulithamini tamasha lao linalotoa ajira kwa Wszanzibar wengi, kukuza uchumi n kuinua hadhi ya Zanzibar kimataifa.

“Ili tamasha ni la kwenu Wazanzibar. Tuliinue tulipende milango ipo wazi kwa wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kulishuhudia na makampuni yajitokeze kulidhamini kwa aina yeyote kwani malengo ya mbele ni kulifanya tamasha hilo la thamani kubwa zaidi” amesema Simai.

ambapo amesisitiza kuwa uwepo wa tamasha hilo si kwa ajili ya kuvutia watalii pekee bali kwa watu wote kwenye nyanja za Utamaduni, mila na desturi za mwafrika kupitia njia ya muziki.

Simai pia amesisitiza kwa vyombo vya habari na wataalamu wa teknolojia ya habari nchini kuendelea kuwaunga mkono katika kutangaza taarifa za habari za tamasha hilo ikiwemo mandhari ya mji wa Zanzibar ili lionekane duniani kote na liwavutie watu wengi duniani kote waje Zanzibar kushuhudia tamasha hilo.

Kwa upande wa Balozi wa Uswis na Norway wanaoziwakilisha nchini zao hapa Tanzania, wamewapongeza Busara Promotions kwa namna wanavyoendesha tamasha hilo ikiwemo kukuza tamaduni za Mwafrika kupitia njia za Sanaa huku wakiahidi kuendelea kudhamini tamasha hilo kwa miaka mingine mingi.

Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Bi. Tinguely Mattli amesema wanaamini tamasha hilo ni moja ya njia ya kufikisha ujumbe kwa wananchi kupitia wasanii ambao wamekuwa ni kioo cha jamii.

Nae Mwakilishi wa Balozi wa Norway nchini na Mkuu wa Idara ya Ushirikiano, Trygve Bendiksby amesema kupitia kauli mbiu ya mapambano dhidi ya rushwa ujumbe utafika kwa wakati na haraka kupitia wasanii.

“Tunaungana na Busara Promotions kwenye tamasha ili kubwa na tutaendelea kulidhamini tamasha kwa kipindi cha miaka mitatu mingine” amesema Bendiksby.

Naye Mkurugenzi wa Busara Promotions, Mahmoud Yusuf amesema kuwa, wamekuwa wakipokea maombi mengi na wengi waliochagliwa wana kiwsngo cha juu.

Yusuf amesema kuwa, wenyeji wamepewa nafasi ya kipekee ya kushuhudia tamasha hilo kwa bei ya ofa maalum kwa siku tsh. 10,000 huku kwa siku zote nne akitakiwa kulipa tsh. 20,000 huku akitaka pia wawe mfano wa kuigwa kwa kuonesha ukarimu na upendo kwa wageni kuanzia vyombo vya usafiri maeneo ya mitaa na manunuzi ili wajisikie wapo na wenyeji wenye moyo wa kupokea wageni.

Naye Meneja waTamasha hilo, Ramadhan Journey alisema kuwa, kwa mwaka huu ni la 16 vikundi 44, vinatarajia kuonyesha burudani kwa siku zote nne kwenye majukwaa matatu tofauti hapo ‘Old Fort’ mjini Stone Town, Zanzibar.

Aidha, Journey ametaja baadhi ya orodha ya Wasanii kwa mwaka huu ni akiwemo, Fid Q kutoka Tanzania Bara, Wasanii wengine na Nchi zao kwenye mabano ni pamoja na: Mokoomba (Zimbabwe), Afrigo Band (Uganda), Fadhilee Itulya (Kenya), Ifrikya Spirit (Algeria), Rajab Suleiman & Kithara ( Zanzibar), Tune Recreation Committee, (Afrika Kusini), Ithrene (Algeria). Hoba Hoba Spirit (Morocco).

Wengine ni M’Toro Chamou (Mayotte/Reunion), Trio Kazanchis (Ethiopia/Switzerland), Faith Mussa (Malawi), Shamsi Music (Kenya), Sofaz (Reunion), Dago Roots( Reunion), Lydol (Cameroun), Jackie Akello (Uganda), S Kide & Wakupeti Band (Tanzania), Tausi Women’s Taarab (Zanzibar), Mkubwa na Wanawe Crew (Tanzania), Damian Soul (Tanzania) na Wamwiduka Band (Tanzania) na wengineo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles