27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Maalim Seif atibua nyongo CCM

MWANDISHI WETU-MOROGORO/ZANZIBAR

SIKU chache baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, kudai kuna njama zinafanya na Serikali na CCM ya kutaka kuimeza kwa maamuzi hatimaye chama hicho kimejibu mapigo.

Hatua hiyo imekuwa baada ya Maalim Seif, kutoa madai hayo kwenye mikutano ya kukagua uhai wa chama Tumbatu, ambapo alikumbusha madai ya kuporwa ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa kudai kwamba ni mipango iliyoratibiwa Tanzania Bara.

Kutokana na madai hayo jana CCM kupitia kwa Katibu wa chama hicho Mkoa wa Morogoro, Shaka Hamdu Shaka, alimjibu Maalim Seif na kudai kwamba kiongozi huyo aache kutonesha vidonda vya Wazanzibari badala yake atubie dhambi ya usaliti aliyomfanyia Hayati Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi .

Shaka, alisema  kama si dhambi hiyo kumtatiza kiongozi  huyo kitambo angeshaukwaa urais wa Zanzibar  na sasa angekuwa katika orodha ya marais wastaafu .

Akizungumza na vijana 60 kutoka katika matawi ya CCM Zanzibar  ambao wako kwenye ziara ya mafunzo mkoani hapa, alisema mwanasiasa anayestahili  lawama ya  kuikwamisha Zanzibar  kisiasa , kidiplomasia au kiuchumi ni Maalim Seif.

Alisema kama si ubinafsi wa kutaka urais kwa pupa, waraka wa Mzee Jumbe ulishajenga nguvu ya hoja ndani ya chama na serikali hivyo mjadala wa muundo wa Muungano na aina  serikali ungemalizika tangu mwaka mwaka 1984.

“Maalim Seif analitia doa jina la Rais Dk. John Magufuli kwa kusaka huruma na umaarufu wa kisiasa. Asikidanganye  kizazi kipya na kuficha usaliti wake. Madai eti Dk. Magufuli ataifanya Zanzibar mkoa ni upuuzi mtupu.

“Ni nani asiyejua kiongozi huyo  endapo ikitokea kushinda urais atairudisha Zanzibar  chini Oman?,” alihoji Shaka 

Alisema anachokifanya Maalim Seif kwa wakati huu ni kuwahadaa wafuasi wake huku akificha ubaya aliomfanyia hayati Jumbe hadi akavuliwa nyadhifa na madarakani yake  kutokakana kile alichodai unafiki na uchonganishi alioufikisha kwa Rais wa kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimu  Julius Nyerere.

“Dk Magufuli hajatamka mahali popote akisema ataifanya Zanzibar  mkoa kwa kuiogopa CUF . Vijana wenzangu ifike mahala tuwe na uthubutu wa kukemea na kulaani mbegu mbaya zinazopandikizwa kwa Taifa.

“Maalim Seif aache kumlisha maneno Mwenyekiti wetu wa CCM Dk. Magufuli . Nadhani muda umefika kwa Maalim Seif kusimama hadharani si vibaya na kuwaomba radhi Wazanzibari kwa kuwafikisha mahali walipo,” alisema

Alisema hata  Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, alipopendekeza iundwe dola moja mwaka 1964 , Mwalimu Nyerere ndiye aliiyekataa wazo hilo  ili isionekane Tanganyika imeimeza Zanzibar.

“Tunaujua mpango wa Maalim Seif akishinda urais atairudisha Zanzibar iwe  chini ya  Oman. Hilo halitatokea  kwani hayupo Mzanzibari yeyote mzalendo  atakayeridhia Zanzibar irudi chini ya Sultan wa Oman hata zipite chaguzi mia asijidanganye hawezi kushinda pamoja na kupita miaka 55 ya Mapinduzi bado Wanzanzibari wana machungu ya kutawaliwa na wakoloni,” alisema Shaka

Katibu huyo aliwataka Watanzania bila kujali itikadi za kisiasa kumpuuza kiongozi huyo kwani madai  hayo  hayana mantiki  na baadala yake

Maalim Seif awatajie wafuasi wake  siku ataapishwa kuwa Rais wa zanzibar kama alivyoahidi na asiikwepe hoja hiyo kwa kuanzisha ingine huku akimzushia uongo na uzandiki  Dk. Magufuli eti ana mpango wa kuifanya Zanzibar

Katibu Mkuu huyo wa zamani wa UVCCM, alisema madai ya kiongozi huyo wakati huu  dhidi ya mkuu wa nchi yamelenga kuvitia hamaki vyombo vya dola ili vimkamate na kumweka kizuizini kwa uzushi na kuhatarisha usalama ili uzuke mtafaruku ambao hauna tija kwa Taifa

“Nadhani wakati umefika kwa Maalim Seif kukaa pembeni na kupisha vijana kuendesha siasa  asome alama za nyakati pamoja na kuwa anaonekana bado ana mkakati wa kutekeleza Azimio la Zanzibar chini ya upinzani kwa mradi wa machafuko.

“Amefilisika kisiasa na mbinu zake kugonga ukuta, ajue hayo ndiyo matunda ya usaliti mwacheni avune kile alichokipanda,” alisema

Kwa upande wao vijana hao kutoka Zanzibar walimshukuru Katibu huyo wa mkoa kwa kuwapokea na kuwapa somo muhimu la historia na namna kukabiliana na wanasiasa ambao wamekuwa vikwazo kwa maendeleo ya nchi kwa kutoa matamko yenye upotoshaji kwa jamii.

CCM ZANZIBAR

Nao Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM),  umesema ukuaji wa demokrasia umetoa fursa pana kwa kila mwananchi kufanya mambo yake kwa uhuru bila usumbufu wa aina yoyote katika jamii.

Akizungumza hivi karibuni Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar,   Mussa Haji Mussa  alisema wanasiasa wanaoilalamikia serikali kuwa imebana demokrasia ni wale waliozoea siasa za vurugu, vitisho na migogoro ya kisiasa hivyo.

“Kwa sasa wanaona hawana tena nafasi ya kufanya matukio ya aina hiyo ndio maana wanalalamika na kueleza bila aibu kuwa Tanzania na Zanzibar kwa ujumla hakuna demokrasia na uhuru wa kutoa na kupokea habari. Pia mpuuzieni huyu mzee anayedai eti kuna mkakati wa kuimeza Zanzibar ameshapoteza dira kwa sasa hana pa kushika,” alisema Mussa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles