30.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

CCM Ileje yaanza kujipanga kuelekea 2024

*Yawapiga msasa Maktibu wa Siasa, Uenezi

Na Denis Sinkonde, Songwe

Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Ileje mkoani Songwe kimewataka Makatibu wa Siasa na Uenezi kuzingatia itifaki katika kutekeleza majukumu yao.

Hayo yamebainishwa leo Mei 26, 2023 na Katibu Mwenezi wa chama hicho Wilaya ya Ileje, Maoni Jeckisoni Mbuba wakati wa ufunguzi wa semina elekezi ya kuwajengea uwezo makatibu hao wa siasa na uenezi ngazi ya kata kutoka kata 8 za wilaya hiyo.

Mbuba amesema lengo kuu la semina hiyo ni kuwajengea uwezo viongozi hao hasa ikizingatiwa uchaguzi umefanyika mwaka jana hivyo wengi wao wanakumbushwa majukumu yao.

Mbuba amesema mafunzo hayo yanatoa dira ya uzalendo kwenye chama kutambua majukumu yao ndani ya chama.

“Viongozi wenzangu nawasihi mafunzo mliyoyapata itumieni kwa kuwa wazalendo na elimu hii mkaieneze ngazi ya matawi lengo ni kuhakikisha wana-CCM wanakuwa imara kuelekea uchaguzi Serikali za Mitaa 2024,” amesema Mbuba.

Aidha, Mbuba amesema kazi ya uenezi si ya kuimba majukwaani tu bali kusimamia miiko na maadili ya chama na kuhakikisha tunaisimamia serikali kutekeleza miradi kwa masilahi mapana ya wananchi.

Mkufunzi CDE Mwalimu Yusuph Ally.

Kwa upande wake Katibu wa Chama hicho wilayani humo, Hassan Lyamba amewasihi mafunzo hayo wayatumie kwa namna walivyofundishwa ikiwa ni mara ya kwanza kutolewa kwa viongozi hao.

“Chama Cha Mapinduzi kinaongozwa kwa kanuni hivyo semina ya leo itawasaidia viongozi hao kujua namna ya kufanya kazi zao ikiwemo kujua masuala ya itifaki katika chama,”amesema Lyamba.

Mmoja wa viongozi hao, Judith Shola amesema mafunzo hayo yamewapa mwanga wa kujua uzalendo wa kukitumikia chama pamoja na kuisemea serikali kwa namna inavyotekeleza kuwaletea wananchi maendeleo.

Makatibu Wenezi, Elimu Malezi na Chipukizi ngazi ya Kata na Tarafa.

Mafunzo hayo yametolewa kwa viongozi hao kutoka kata ya Kafule, Ikinga, Malangali, Ngulugulu, Sange, Lubanda, kalembo na Luswisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles