24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Shule za Ibun Jazar zawafunza vijana maadili mema

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wazazi weshauriwa kuwapelekea vijana wao kwenye shule za Ibun Jazar kwani shule hizo ni za Kiislam na zenye malengo ya kutoa elimu yenye maadili mema.

Mkurugenzi wa Shule hizo, Sheikh Othman Ali Kaporo alisema jijini Dar es Salaam hivi karibuni kuwa shule hizo malengo yake ni kutoa elimu bora kwa vijana inayoambatana na maadili mema.

“Shule hizi zina mlengo ya  kuwalea watoto katika maadili mema  kupitia a kitabu cha Quran tukufu na  hivyo basi zimeweza kutoa vijana wengi wenye maadili mema na wakati huo huo wakiwa na kiwango cha elimu chenye kuridhisha,” anasema.

Anasema kuwa mafanikio yote hayo yametokana na juhudi za watendaji wakuu wa taasisi wakiwamo walimu wakuu, mameneja wa shule za Ibun Jazar katika kufikisha ujumbe na elimu bora kwa vijana.

“Ibun Jazar ni miongoni mwa watu wanaochangia kuzalisha nguvu kazi imara, ulimwengu hivi sasa unalia na vitu sana miongoni mwavyo ni watu kupokea rushwa katika baadhi ya taasisi,” anasema .

Meneja wa Shule ya Sekondari Ibun Jazar.

Kutokana na hilo anasema taasisi yake inale vijana na kuwafundisha kuwa rushwa ni adui wa haki na ni dhambi mbele ya Mwenye zi Mungu kutoa au kupokea rushwa .

Anafafanua kuwa, malezi haya ya kiroho na kiimani ndiyo vitu pekee vinavyoweza kuisaidia jamii kuwa na maadili mema hivyo naiomba jamii tushirikiane ili kujenga jamii bora ya Kitanzania.

Naye na Meneja wa Shule ya Sekondari ya Ibun Jazar Mtoro Bakari anasema kuwa shule hizo vijana wanahifadhi Quran tukufu wanafundishwa elimu ya dini na masomo ya kawaida.

“Kikubwa ambacho tunaomba umma ufahamu ni kwamba tunawafundisha vijana kuwa na maadili mema ili wanapotoka hapa kwenda kulitumikia taifa wawe ni vijana wenye maadili mema kwa taifa lao,” amesema.

Anasema pia kuwa utafiti umeonyesha kuwa vijana anapofundishwa kuhifadhi Quran tukufu basi hata uwezo wake wa kuelewa masomo mengine unakuwa mkubwa.

Shule ya Msingi Ibun Jazar na Sekondari zipo Vikindu Wilaya Mkuranga Mkoa wa Pwani na hadi sasa zimeshasomesha vijana wengi ambao wamemaliza vyuo vikuu mbalimbali na kwa sasa taasisi hiyo inasomesha vijana wengine katika vyuo vikuu mbalimbali.

Jengo la Shule ya Sekondari Ibun Jazar.

Akizungumzia matokeo ya mwaka jana kidato cha nne anasema katika watahiniwa 69, waliofaulu kwa daraja la kwanza walikuwa 58 na daraja la pili 11.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles