20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Picha|’Ni Wananchi na Rais Samia Dar’

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Klabu ya Yanga maarufu ‘Wananchi’ wameendelea kuunga mkono kile kinachofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan cha kutoa motisha kwa timu yao pindi inapofanya vizuri.

Ikumbukwe kuwa Yanga kesho Jumapili Mei 28, 2023 itashuka katika dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam kuvaana na USM Alger’s ya Algeria katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho Barani.

Mashabiki hao kutoka matawi ya tawi la Mwananyamala, Kidali Asilia, Tandale wamempongeza wakiwa na mabango mbalimbali yenye picha na jumbe tofautitofauti wameendelea kumsifia Rais Samia kwa hamasa aliyoiweka katika michezo hadi kuwezesha klabu hiyo kufika hatua ya fainali kombe la Shirikisho barani Afrika.

Ikumbukwe kuwa katika michezo miwili ya fainali ya Shirikisho Rais Samia ameahidi kutoa Sh milioni 20 kwa kila goli iwapo Yanga itaibuka na ushindi.

Kama hiyo haitoshi, Rais Samia amesema Serikali itatoa ndege ya kuipeleka Yanga nchini Algeria kwenye mchezo na wa marudiano utakaopigwa Juni 3, ambayo itaisubiri na kisha kuirejesha nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles