23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Washiriki Sabasaba waongezeka

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Idadi ya washiriki wa Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba (DITF) imeongezeka hadi kufikia 1,317 ndani na nje ya nchi.

Akizungumza Mei 26, jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Biashara TanTrade, Fortunatus Mhambe amesema kati ya kampuni hizo 1,203 ni za ndani na 114 ni za nje.

“Nchi 14 zimeomba kushiriki katika maonyesho haya ya 47 nchi hizo ni pamoja na China, Umoja wa Falme za nchi za Kiarabu (UAE), Uturuki, Kenya, Ghana, India,Singapore, Syria, Iran, Indonesia, Rwanda, Algeria na Pakistan,” amesema Mhambe.

Naye Katibu Mtendaji wa Taasisi Binafsi Biashara za Madini, Injinia Benjamin Mchwampaka amesema kuhusu sabasaba ExpoVillage litakuwa ni banda moja ambalo litakuwa na mambo mengi yanayo husika na madini kwa ujumla ikiwa tofauti na miaka mingine kila mtu anakuwa na banda lake.

Naye Mkurugenzi wa Tanzakwanza Stragists, Francis Daudi amesema lengo la kampuni yao wanataka kutangaza furusa zipi? zinapatikana nchini huduma na rasilimali watu.

“Kuna umuhimu wa kuleta teknolojia mpya ili kuonyesha maonyesho ya sabasaba kutambua mchango wa sekta, taasisi na kampuni zilizofanya vizuri katika maonyesho haya,” amesema Francis.

Amesema kutakuwa na siku maalumu ya madini katika sekta 8 wadau wanataka kuwekeza kwenye madini watakutana kujadili changamoto.

Naye Afisa Mradi wa Mfuko Unasaidia Wajasiriamali kutoka Vijijini, Bertha Kageuka amesema kuwa zaidi ya wanawawake 50 Wajasiriamali kutoka mikoa mbalimbali watashiriki maonyesho wengi wa bidhaa nzuri na wanatoa elimu kuboresha bidhaa na nembo ya biashara. Kwa upande wake Afisa Mwandamizi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Latiffa Kigoda amesema lengo ni kuhamasisha wawekezaji sekta zote nchini kwa wazawa na wageni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles