30.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mnada wa Chai kuanza Juni jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi wetu, Dodoma
WAZIRI wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe amesema kuwa mnada wa Chai unatarajiwa kuanza mwezi Juni mwaka huu ambapo mara baada ya kuanza hakuna mtu atakayeruhusiwa kuuza chai nje ya mipaka ya Tanzania.
.
Bashe ameyasema hayo Mei 21,2023 jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya siku ya Chai Dunaini kitaifa na kusema kuwa awali mnada huo ulikua uanze mwezi Desemba.
 
Amesema kuwa Chai yote ya Tanzania ni lazima ipite kwenye mnada na wanunuzi wa ndani watanunua chai mnadani hata kama wana mikataba ya manunuzi.
 
Bashe amesema ambaye hatataka kupitisha chai mnadani hakuna kupewa kibali cha kusafirisha chai kwenda nje.


 
Aidha Waziri Bashe amezitaka kampuni zinazonunua chai kutoka kwa wakulima hapa nchini kuhakikisha wanawalipa wakulima hao kwa wakati kwani si vyema kwa wanunuzi kuchukua majani ya chai kutoka kwa mkulima halafu hawawalipi.
.
“Nina data hapa, kuna kampuni inadaiwa malipo ya pili toka mwaka 2018 haijawalipa wakulima sasa nimemuagiza DG kuanzia sasa ataanza kuwapiga faini. Hiyo ni haki ya wakulima kwa sababu mmechukua hela ya wakulima mmekaa nayo, mnatakiwa kulipa” Amesema Bashe.
 
Ameziomba sekta binafsi kujitokeza kwenye mnada huo utakao fanyika jijini Dar es Salaam kwa sababu hauna athari yoyote kwenye biashara zao.
 
Mapema akimkaribisha Mgeni rasmi kuzungumza na wadau wa Chai katika maadhimisho hayo ya Siku ya Chai Duniani, Mkurugenzi wa Bodi ya Chai Tanzania Bi. Mary Kipeja alisema uzalishaji wa chai hapa nchini bado una udumavu mkubwa ukilinganisha nan chi nyingine za ukanda wa Afrika Mashariki zinazolima Chai.
 
Kipeja amsema wao kama wadau wakubwa kwa sasa wanajikita katika kuimarisha soko la ndani ambalo kwa sasa ni asilimia 15 na wanataka kulifikisha asilimia 30, ili watanzania waweze kutumia chao wenyewe.
 
amewaomba wadau wote wa tasnia ya chai waweze kushirikiana na bodi hiyo ili kuweza kufanya mapinduzi makubwa ya zao la chai na kuweza kupata manufaa mbalimbali kama kuzalisha ajira na kupata kipato kwa ajili ya kuongeza pato letu la taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles