24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Makatibu wa Afya nchini watakiwa kusimamia vizuri miradi ya afya

Na Clara Matimo, Mwanza

Makatibu wa Afya nchini wametakiwa kusimamia vizuri miradi ya afya inayotekelezwa na Serikali kwenye maeneo yao ili malengo yaliyokusudiwa yaweze kufikiwa na ikamilike kwa wakati.

Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana akizungumza wakati akifunga mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Makatibu wa Afya Tanzania uliofanyika mkoani humo kuanzia Mei 16 hadi 19,2023.

Pia wametakiwa kusimamia kwa weledi Mifumo ya Ukusanyaji Mapato kwenye Maeneo yao ya kazi ili fedha zitakazopatikana ziisaidie serikali kutatua changamoto zilizopo kwenye maeneo hayo na hivyo kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi ambalo ndiyo lengo kuu la serikali.

Wito huo umetolewa juzi jijini Mwanza na Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Balandya Elikana wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Makatibu wa Afya Tanzania uliofanyika mkoani humo kuanzia Mei 16-19, 2023 ukiwa na kauli mbiu ‘Uwekezaji na uimarishaji wa mifumo ya afya nchini ni msingi wa utoaji huduma bora kwa wananchi’.

“Ili tuweze kulitumikia taifa letu ni vizuri tuwe na afya njema, tukiwa na afya njema tutafanya kazi tukiwa na nguvu kubwa na hivyo kutimiza malengo yetu na nchi ili hayo yatimie nyie makatibu tawala mnayo nafasi kubwa sana katika utendaji kazi wenu.

“Mkisimamia vizuri miradi ya afya ikakamilika kwa wakati na ikiwa na thamani halisi ya fedha pia mkisimamia vizuri mifumo ya ukusanyaji mapato kwenye maeneo yenu ya kazi adhima ya serikali itatimia ya kutoa huduma bora za afya kwa wananchi maana fedha hizo zitatumika badala ya kusubili zitoke serikali kuu,” alisema Elikana.

Elikana aliwataka pia makatibu hao wa Afya kwenda kusimamia upatikanaji wa takwimu sahihi katika kutoa maamuzi ili kuweka uhalisia wa ushughulikiaji wa masuala mbalimbali katika sekta ya afya.

“Imani yangu ni kwamba siku nne mlizokuwepo hapa mmepeana hamasa na chachu ya kuongeza bidii na kuwezesha utoaji wa huduma bora hivyo natumaini mtaenda kuboresha huduma za takwimu kwenye maeneo yenu ya kazi,” alisisitiza Balandya.

Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Thomas Rutachunzibwa, Muuguzi Mkuu wa Mkoa huo Claudia Kaluri aliwataka makatibu afya hao kwenda kutekeleza kwa vitendo malengo waliyojiwekea ikiwemo kushirikisha kada na idara zingine kuongeza uwazi na uwajibikaji na kufanya maamuzi kwa pamoja ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama hicho Juliana Mawala aliwataka makatibu hao kutofanya kazi kwa mazoea bali wabadilike kulingana na mahitaji ili kuboresha zaidi utendaji wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles