22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Tax azindua mfumo wa kusajili Diaspora Kidigitali

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stergomena Tax amezindua mfumo maalumu wa kidigatal wa kusajili Daispora wenye asili ya Tanzania wanaoishi nje ili kuweza kutatua changamoto zinazo wakabili.

Akizungumza leo Dar es Salaam Mei 22, wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali kutoka serikalini, sekta binafsi na wadau, Waziri Dk. Stergomena amesema jukumu la wizara ni kusimamia na kuweka mifumo thabiti kwa ajili ya Diaspora wanaoishi nje.

“Kwa miaka mingi balozi wamekuwa wakisajili Daispora katika masuala mbalimbali na mwitikio umekuwa mdogo wengine kushindwa kujisaji na kufika balozini gharama ni kubwa wapo mbali na balozi, sababu mbalimbali kupitia mfumo huu wa kidigatal utasaidia daispora kujisajili mahali popote duniani,” amesema Dk. Stergomena.

Amesema kuwa mfumo huo waliojisajili utawasaidia kupata taarifa za kiuchumi na kijamii taarifa hizo kuwafikia kwa wakati diaspora ni maalumu kujiandikisha.

Amesema matarajio ya serikali ni kuwasajili diaspora wote kupata kazi data sehemu waliopo ulimwenguni ikiwemo kupata kazi na kuwapata kwa wepesi watoa huduma nchini kama benki, vitambulisho vya taifa na vinginevyo.

“Kuhakikisha watakao jiunga na mfumo huu umezingatia sheria ya usalama wa taarifa binafsi, kudhiti uhalifu wa mitandaoni na sheria hizi zimezingatiwa niwatoe wasi wasi,” amesema Dk. Stergomena.

Amesema elimu kwa umma itolewe kwa haraka ili mtu aweze kuelew lazima mtoe elimu na madaispora mliopo hapa mkawe mabalozi wazuri kuwaambia wenzenu ni kweli tumezindua mfumo huo.

Aidha, amesema suala la uraia pacha ni moja ya kazi maalumu ya hotuba ya Mei 30 mwaka huu.

Nae Kamishina Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala amesema kuanzishwa kwa mfumo huo utasaidia kupata vibali kama hati ya kusafiria na visa.

“Kusaji Daispora kuna faida nyingi ikiwemo kuwezesha kapata huduma na furusa, kulalamikia changamoto zinazo wakabili na kuwafikishia huduma hasa za uhamiaji kwa wakati,” amesema Dk. Anna.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya CRDB, Abdulaziz Nsekela amesema kuwa wameunganisha mfumo huo kwenye website zao diaspora watapata huduma za kibenki zote ikiwemo kufungua akaunti na zinginezo.

Upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB, Philbert Mponzi amesema kupata taarifa kamili za diaspora wanaoishi nje na kupitia banki hiyo watapata huduma nzuri na kushiriki maendeleo ya nchi.

Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba amesema mfuko wa NSSF upo kisheri na kuwasaidia daispora kila nchi ina mfumo wa kuchangia hifadhi ya jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles