31.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga kuimaliza Simba Pemba

DSC1488NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

TIMU ya Yanga ya Dar es Salaam imepanga kuwamaliza wapinzani wao Simba mapema kwa kuamua kuweka kambi Pemba kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao ya watani wa jadi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, itakayochezwa katika Uwanja wa Taifa, Februari 20.

Yanga itatua Pemba mara baada ya kumaliza mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Cercle Joachim ya Mauritius, utakaochezwa Jumamosi hii katika Mji wa Curepipe.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, ofisa habari wa klabu hiyo, Jerry Muro, alisema mchezo wao dhidi ya Cercle watautumia kujiandaa dhidi ya mahasimu wao Simba.

“Baada ya kumalizika mchezo wa kimataifa siku hiyo hiyo tutasafiri hadi Pemba kuanza kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba Jumamosi ijayo.

“Tukimaliza mchezo wa Simba, tutarudiana na Cercle De Joachim kabla ya kukutana na timu ya Mtibwa Sugar, hivyo kufanya ratiba yetu kuwa ngumu zaidi katika kipindi hiki,” alisema Murro.

Akizungumzia juu ya safari yao ya Mauritius, alisema watatumia ndege ya kukodi ya Air bus, ambayo itatumika kusafirisha wachezaji, wakuu wa msafara pamoja na viongozi wa klabu  hiyo kesho.

Yanga jana ilitangaza kughairisha safari ya Mauritius ikieleza kuepuka hujuma dhidi yao nchini Afrika Kusini.

Alieleza uamuzi huo wa ghafla ulitokana na uchunguzi uliofanywa na ‘intelijensia’ ya timu hiyo na kubaini kampuni ya ndege ya Mauritius Airways ambayo ingetumika kuwasafirisha, ilipanga kuwachelewesha zaidi ya masaa saba uwanja wa ndege hali ambayo ingeharibu utayari wa wachezaji.

“Hatukuwa na jinsi baada ya kugundua mipango michafu dhidi ya wapinzani wetu kwa kuwa dhamira yetu ni kupata ushindi, hivyo tuliamua kuvunja kibubu na kukodi ndege binafsi.

“Baada ya kufika tutafanya mazoezi uwanja ambao tutatumia kwa ajili ya mchezo wetu Jumamosi hii, katika Mji wa Curepipe nchini Mauritius,” alisema Murro.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles