31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Yona: Tutatumikia adhabu yetu kikamilifu

2.Yona-akiwa-ameshika-fagio-na-fyekeo-atakalofanyia-usafi-katika-Hospitali-ya-Parestina.Na Grace Shitundu, Dar es Salaam

WAZIRI wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona, amesema yeye na mwenzake Basil Mramba ni watiifu na watatumikia adhabu yao kikamilifu pasipo kukiuka sheria.

Yona na Mramba aliyekuwa Waziri wa Fedha, wanaendelea kutoa huduma za kijamii katika Hospitali ya Sinza Palestina, Dar es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa adhabu ya kifungo cha nje waliyoanza kuitumikia wiki hii.

“Hii ni adhabu na tutahakikisha tunaitekeleza kikamilifu pasipo kukiuka sheria za nchi, tunaendelea na majukumu kama kawaida,” alisema Yona alipozungumza na MTANZANIA jana hospitalini hapo baada ya kumaliza kupiga deki na kufagia.

Kwa upande wake, Mramba alisema wako tayari kuhudumia jamii katika hospitali hiyo kwa kila jambo, hata kama watahitaji huduma ya kitaaluma wako tayari kutoa.

“Tunaendelea na majukumu na tuko tayari kushirikiana na utawala hata kwa mambo ya kitaaluma. Kwa mfano sisi wengine ni wachumi tunaweza kuwasaidia masuala ya kupanga bajeti,” alisema.

Mawaziri hao wa zamani walifika hospitalini hapo mapema kabla ya saa mbili na kumsubiri msimamizi wao ambaye ni Ofisa Mazingira wa hospitali hiyo, Mariamu Mongi kuwapangia kazi za kufanya.

Mongi aliwaelekeza kazi ya kufanya ambapo walikabidhiwa vifaa na kuanza kupiga deki katika ngazi zinazopandisha kwenda kwenye wodi ya wazazi na baada ya kumaliza shughuli hiyo, walishuka na kufagia nyuma ya jengo hilo.

Siku ya jana, hali ilikuwa tofauti na siku zilizopita ambapo mawaziri hao walifanya kazi pasipo kuzingirwa na watu.

Ilipofika saa 4:30 asubuhi, mawaziri hao wa zamani walimaliza kazi walizopangiwa, kisha wakaelekea kwa ofisa mazingira ambapo walikaa kwa zaidi ya dakika 45.

Ofisa huyo alisema ratiba inaonyesha mawaziri hao wa zamani leo watasafisha vioo katika jengo la huduma za wagojwa wa nje (OPD).

“Wanafanya kazi hizi kwa kuwa wagonjwa ni wengi, kazi ya kufyeka wataifanya siku ya Ijumaa kwa sababu wagonjwa wanakuwa wachache,” alisema Mongi.

Alisema watakuwa wanafanya kazi kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles