26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kabila awazawadia wachezaji magari ya kifahari

Congo-DC-playersKINSHASA, CONGO

RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila, amewazawadia wachezaji wa timu ya Taifa nchini humo magari ya kifahari baada ya kushinda Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN).

Rais huyo ametoa zawadi ya gari kwa kila mchezaji aina ya Toyota Prado, lenye thamani zaidi ya milioni 120, pamoja na medali kwenye hafla iliyoandaliwa katika Ikulu jijini Kinshasa nchini humo.

Hata hivyo, nahodha wa timu hiyo, Joel Kimwaki na kocha Florent Ibenge, wao wamepewa magari aina ya Ranger ambayo ni tofauti na magari mengine ambayo yametolewa kwa wachezaji.

“Asanteni sana kwa ushindi huu, kujituma kwenu na kufanikiwa kuchukua ubingwa kunaleta amani na uimara wa nchi yetu.

“Tunaweza kusema kwamba nchi kwa sasa ipo katika mshikamano na umoja, kama vile ambavyo mlishikamana katika hatua ya mwanzo hadi mwisho wa michuano hiyo,” alisema Kabila.

Timu hiyo ilifanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa kuwalaza Mali mabao 3-0, kwenye fainali ambazo zilipigwa mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Rwanda na kuwa Taifa la kwanza kushinda kombe hilo mara mbili.

Mwaka 2009, mara ya kwanza kuandaliwa kwa michuano hiyo, DR Congo waliondoka na ubingwa kwa kuwafunga Ghana ‘Black Stars’ mabao 2-0.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles