25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Mayanja akubali jeshi la Mfaransa Stand Utd

Mayanja-J-1NA JUDITH PETER, DAR ES SALAAM

KOCHA Msaidizi wa Simba, Mganda Jackson Mayanja, amekiri kuwa kikosi cha wapinzani wao Stand United kimebadilika tofauti na msimu uliopita, hivyo wana kazi kubwa ya kupambana ili kupata pointi muhimu ugenini.

Simba ambao wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wanarajia kushuka dimbani Jumamosi hii kuchuana vikali na wenyeji wao Stand United katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Msimu uliopita Simba ilishindwa kufurukuta mbele ya Stand United walipokutana katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 kabla ya kupokea kipigo cha bao 1-0 ugenini waliporudiana katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mayanja alisema katika soka mambo yanaweza kuwa tofauti wakati wowote hasa unapocheza katika uwanja wa ugenini, hivyo anategemea mabadiliko na si ushindi wa mabao mengi kama ilivyokuwa mechi zilizopita.

Alisema hawafahamu vizuri wachezaji wa Stand United, huku akikiri kuwa kikosi hicho kina mabadiliko makubwa msimu huu chini ya kocha Mfaransa, Patrick Liewig, tofauti na msimu uliopita ambao hawakufanya vizuri sana.

Mayanja mwenye uzoefu mkubwa katika michuano ya Ligi Kuu Bara kutokana na kuifundisha Kagera Sugar kwa muda mrefu kabla ya kuinoa Coastal Union mwanzoni mwa msimu huu, alisema wachezaji wake wapo fiti na wanaendelea na mazoezi kujiandaa na pambano la keshokutwa.

“Wachezaji wote wapo katika hali nzuri hakuna ambaye ni majeruhi, wote wanaendelea na mazoezi kuhakikisha tunaendeleza kasi yetu na kuibuka na ushindi ili kujiongezea pointi muhimu,” alisema.

Alisema hawafahamu vizuri wachezaji wa Stand United, lakini kikosi hicho kina mabadiliko makubwa msimu huu tofauti na msimu uliopita ambao hawakufanya vizuri sana.

Mayanja amekuwa na mafanikio makubwa ndani ya kikosi cha Simba tangu aanze kukinoa mwishoni mwa mzunguko wa kwanza wa ligi, ambapo tayari ameshinda mechi tano mfululizo na kuipandisha hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles