26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 5, 2023

Contact us: [email protected]

50 Cent amgeukia mwingine anayemdai

LOS ANGELES, Marekani

ALIANZA na mwigizaji aitwaye Rotimi, ambaye alisema aliwahi kumkopesha Dola za Marekani 300,000, kabla ya baadaye kuibuka na madai kuwa wamemalizana.

Safari hii, 50 Cent amedai kuwa anamdai rapa wa Kundi la G-Unit, Tony Yayo, akisema aliwahi kumkopesha kiasi cha mkwanja.

Hata hivyo, katika majibu yake dhidi ya deni hilo, Yayo alisema awali alidhani ni zawadi na si kukopeshwa kama anavyodai Cent.

“Hukuniambia nikulipe!” alisema Yayo na kuongeza: “Sisi ni marafiki. Unazungumzia nini?”

Katika majibu yake, Cent alisema: “Sina marafiki, nakupenda kijana lakini unatakiwa kunirudishia mpunga wangu.”

Kile walichokikosa waandishi wa udaku ni kwamba Cent hakuweka wazi kiasi cha fedha anachomdai mshikaji wake huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles