26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mtoto wa Jenner akimbizwa hospitali

LOS ANGELES, Marekani

HABARI mbaya kwa mashabiki wa mrembo wa vipindi vya trelevisheni anayetokea familia ya Kardashian, Kylie Jenner, ni kwamba juzi mtoto wa binti huyo alikimbizwa hospitali.

Hata hivyo, Kylie mwenye umri wa miaka 21 amedai kuwa Stormi mwenye umri wa miezi 15 alifikishwa kwa madaktari akisumbuliwa na wa mzio (allergy) na amesharejea nyumbani.

Kuwataarifu mashabiki wake, Kylie aliposti picha katika mitandao ya kijamii, ikimuonesha dogo huyo akiwa amelala.

“Nilitumia siku nzima nikiwa hospitali na mtoto wangu. Alikuwa na tatizo la mzio lakini yuko sawa kwa asilimia 100 na sasa tuko nyumbani,” alisema bibiye huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles