25.3 C
Dar es Salaam
Thursday, December 2, 2021

TPB yatoa msaada wa saruji mifuko 100

MWANDISHI WETU,SENGEREMA

BENKI ya TPB tawi la Sengerema mkoani Mwanza, imetoa msaada wa mifuko 100 ya saruji yenye thamani ya Sh milioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Busisi.

Msaada huo ulikabidhiwa mwishoni mwa wiki na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi, kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Boniface Magesa.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Moshingi alisema benki hiyo ilitoa msaada huo kama sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake katika jamii.

“Benki ya TPB ina wateja zaidi ya 6,000 waliomo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ambao wamefikiwa na huduma zetu.

“Katika uendeshaji wa benki yetu, huwa tuna utaratibu wa kutenga moja ya faida kila mwaka kwa ajili ya kuisaidia jamii katika masuala mbalimbali, yakiwemo ununuzi wa madawati shuleni, ujenzi wa maabara, kuchangia sekta ya afya, kutoa pole kwa waliopatwa na majanga katika sekta ya elimu,’’ alisema Mishingi.

Naye Magesa, alisema TPB imekuwa msaada kwa wananchi kwa huduma inazotoa.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Busisi, Mark Dominiki, alisema msaada huo utawasaidia kukabiliana na uhaba wa madarasa uliokuwa ukiwakabili.

“Shule yetu ina jumla ya wanafunzi 1,098 ambao wanatumia madarasa 7 tu, kwa msaada huu kutoka TPB utatupunguzia uhaba huu kwa kuongeza ujenzi wa madarasa mengine,’’ alisema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,639FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles