26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Neymar avuliwa unahodha Brazil

SAO PAULO, BRAZIL

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar, amevuliwa unahodha wa kuiongoza timu hiyo kwenye michuano ijayo ya Kombe la Copa America, huku nafasi hiyo ikitajwa kuchukuliwa na Dani Alves.

Michuano hiyo msimu huu inatarajiwa kufanyika kwenye ardhi ya Brazil kuanzia Juni 14 hadi Julai 7, zikijumuisha timu 12 kutoka Amerika ya Kusini.

Neymar, ambaye anakipiga katika klabu ya Paris Saint-Germain pamoja na Alves, alitajwa kuwa nahodha wa kudumu wa kikosi hicho, chini ya kocha wao, Tite, tangu alipomchagua Septemba 2018, lakini sasa amevuliwa nafasi hiyo na badala yake kupewa Alves, mwenye umri wa miaka 36.

Shirikisho la Soka la Brazil (CBF), liliweka wazi taarifa hiyo mara baada ya kocha huyo kufanya mazungumzo na Neymar mwenyewe.

“Maamuzi hayo yamefanywa baada ya kocha Tite kuzungumza na Neymar, hivyo kila kitu kipo sawa, kwamba Dani Alves atachukua nafasi hiyo kwenye michuano ya Kombe la Copa America kwenye ardhi ya nyumbani,” waliandika.

Hatua hiyo ilianza katika klabu yake ya PSG, ambapo Neymar alivuliwa kitambaa hicho na kocha wake, Thomas Tuchel, baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Msimu huu Neymar amefunga jumla ya mabao 23 kwenye michuano mbalimbali, kati ya mabao hayo, 15 amefunga kwenye michuano ya Ligi Kuu Ufaransa (Ligue 1).

Neymar, mwenye umri wa miaka 27, amekuwa akihusishwa kutaka kuondoka katika klabu yake ya PSG msimu huu, kuna taarifa kwamba lengo lake kubwa ni kurudi nchini Hispania katika klabu yake ya zamani ya Barcelona au Real Madrid.

Hata hivyo, Rais wa Madrid, Florentino Perez, ameweka wazi kuwa hawana mpango wowote wa kutaka kumsajili mchezaji huyo katika kipindi hiki cha kiangazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles