31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Perez awakataa Mbappe, Neymar

MADRID, HISPANIA

RAIS wa timu ya Real Madrid, Florentino Perez, amesisitiza kuwa, uongozi wake hauna mpango wowote wa kuwasajili nyota wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe na Neymar.

Siku za hivi karibuni wachezaji hao wameripotiwa kuwa wanataka kuondoka katika klabu yao, hivyo mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Ulaya walitajwa kutaka kuvunja benki yao kwa ajili ya wachezaji hao.

Baada ya Real Madrid kushindwa kufanya vizuri msimu huu, Zinedine Zidane aliweka wazi kuwa anataka kuongeza wachezaji kwa ajili ya kuleta ushindani msimu ujao.

Msimu huu uliomalizika siku za hivi karibuni Madrid ilimaliza kwenye nafasi ya tatu katika Ligi Kuu Hispania, huku Atletico Madrid wakimaliza nafasi ya pili na Barcelona wakitwaa ubingwa. Hata hivyo, Madrid waliondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora dhidi ya Ajax.

“Sijawahi kufanya mazungumzo yoyote na kocha Zidane juu ya kuwasajili nyota wa PSG, Mbappe au Neymar na sina mpango wa kuwazungumzia wachezaji hao kwa kuwa hatuna mipango nao.

“Mwaka jana tuliweka wazi kuwa hatuna mpango na wachezaji hao na hata mwaka huu tunasema hivyo hivyo kuwa hatuna mpango huo. Kama tutakuwa tunawahitaji basi tutafanya mazungumzo na uongozi wa klabu yao,” alisema rais wa timu hiyo.

Real Madrid kipindi hiki cha usajili wa kiangazi wanahusishwa kutaka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard. Tayari mchezaji huyo ameweka wazi kuwa mchezo wa leo wa fainali ya Kombe la Europa utakuwa wa mwisho kuitumikia klabu hiyo ya Chelsea.

Chelsea leo watashuka dimbani dhidi ya wapinzani wao, Arsenal, kwenye fainali hiyo, hivyo Hazard amewaaga wachezaji wenzake huku akisema ndoto zake kubwa ni kwenda kucheza soka la kulipwa katika klabu hiyo ya mabingwa wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid.

Hata rais wa Madrid jana aliweka wazi kuwa watahakikisha wanaipata saini ya mchezaji huyo katika kipindi hiki cha kiangazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles