25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Nape: Sipingani na JPM

*Aeleza sababu ya kujiuzulu uenyekiti kamati ya Bunge

ASHA BANI-DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Mtama, Nape Nnauye (CCM), amesema hampingi Rais Dk. John Magufuli waka serikali katika kutekeleza miradi, bali anapingana na namna ambavyo inaendeshwa.

Pamoja na hali hiyo amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya ya utekelezaji wa miradi hiyo ambayo alieleza inahitaji ujasiri na msimamo usiyoyumbishwa.

Kauli hiyo ya kwanza ya Nape, aliitoa mwishoni mwa wiki katika mahoaji maalumu kupitia Redio A FM ya jijini Dodoma, ambapo alisema yeye ni mmoja walioshiriki katika kuandika Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015.

Alisema miradi inayotekelezwa sasa ilikuwemo hivyo hana haja ya kupinga bali anatoa hoja katika maboresho.

“Sipingani na serikali katika kutekeleza miradi yake bali namna gani inavyoendeshwa ndio mjadala ambao nasema tunaweza kuzungumza.

“Tumeanza na mradi wa ndege pale tumenunua kwa fedha za serikali lakini hii ndio njia pekee ambayo mwingine anaweza kuamini hivyo na kupishana namna ya kutengeneza,  sio jambo baya na tungepishana katika miradi yenyewe ingekuwa jambo tofauti sana lakini tunapishana katika utekelezwaji,” alisema Nape.

Alisema pamoja na kushiriki katika kutengeneza ilani ya uchaguzi miradi hiyo mingi ipo kwenye ilani ila kwa sasa ni namna kutekeleza wake ndio mjadala uliopo mitaani.

Alisema hakuna haja ya kuua huo mjadala na si kwamba mtu akijadili aonekane anapinga jambo ambalo si kweli na  anafanya hivyo katika kupata jambo bora na ni vizuri kuzungumza.

“Kwa hiyo nasema mimi naunga mkono na kazi hii Rais  anafanya ni lazima kua na ujasiri kua na msimamo lakini si vibaya watu wakajadili namna inavyotekelezwa kwa sababu nchi ni ya kwao na fedha za kwao.

“Leo kwa mfano nataka kujenga barabara ya Dar es Salaam kuelekea Dodoma huko kwengine duniani tungeweza kutandaza laini nane lakini akaja mwekezaji binafsi wakajenga halafu wakatoza fedha za ushuru wa barabara likawezekana ,” alisema Nape.

Alisema kama mpaka sasa wangetaka kujenga daraja la Kigamboni kwa fedha za serikali isingewezekana kwa kuwa mkakati huo ulikuwapo tangu enzi za utawala wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, lakini ulichelewa ila baada ya kupewa kazi hiyo mashirika mradi huo wa ujenzi umekamilika.

“Juzi napita pale darajani Kigamboni nalipia lakini wakati natoa fedha naona naambiwa hapana wabunge hawalipii nalo nikashangaa, wakati sisi ndio wenye hela tulipaswa kulipa maana wanalipia mpaka wauza madafu pale nikampa hela nikamwambia lete risiti,” alisema Nape

Alisema amekuwa wa kwanza na muumini wa kuipa nafasi sekta binafsi lakini kama serikali imeamua kufanya wenyewe yeye hana tatizo mwisho wa siku anapata huduma kama ambavyo anapata katika ndege hizo za serikali.

KUHUSU KUJIUZULU

Apoulizwa sababu za yeye kujiuzulu uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili na Utalii, alisema alichukua uamuzi huo kwa lengo la kujipa nafasi ya kuweza kuhudumia jimbo kwa kuwa muda uliobaki ni mdogo kati ya alioomba wa miaka mitano.

“Nimejiuzulu ili nikafanye kazi jimboni mijadala yote inayoendelea itakuja tu na niseme kwamba kujiuzulu kwangu kunaweza kuwa na sababu nyingi lakini kubwa mjue  ile niliyoandika katika barua na kumpa Spika ni yenyewe hayo mengine nawaacha watu wajadili,” alisema Nape.

MSIMAMO JUU UMILIKI ARDHI

Nape alisema yeye ni mtu wa kwanza kutengeneza ilani ya uchaguzi na alisema kama kuna watu wamemilikishwa ardhi na wameshindwa kuiendeleza ni vizuri ukatumika utaratibu wa kuzungumza nao na sheria zikafuatwa .

“Nasisitiza wale waliochukua mmashambamakubwa mno kuliko uwezo wao wa kushindwa kuendelezwa yachukuliwe wapewe wengine ili yasibaki mapori sasa mjadala juu nani ananyang’anywa ni mpana lakini nchi inafuata sheria tusimuonee mtu ,” alisema

Wiki iliyopita Nape, alichukua uamuzi wa kujiuzulu Uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili na Utalii.

Hata hivyo hatua hiyo ilidaiwa kutokana na kuwa na msimamo kuhusu baadhi ya mambo kutokwenda sawa kwenye sekta ya ardhi hasa kwa wawekezaji wa mashamba.

Kujiuzulu kwake, kunatokana kilichodaiwa ni “Kugoma kuondoa taarifa ya uchukuaji wa mashamba ya wawekezaji”.

Taarifa kutoka ndani ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii zinasema, Nape amejiuzulu baada ya kutofautiana na serikali kuhusu ripoti ya kamati yake aliyokuwa akiiongoza.

Taarifa kutoka ndani ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii zilinukuu taarifa ya Nape kumwandikia barua rasmi ya Spika kumjulisha kujiuzulu kwake.

Machi mwaka 2017, Nape aling’olewa kwenye nafasi ya uwaziri wa habari, utamaduni, Sanaa na michezo.

Mbunge huyo wa Mtama mkoani Lindi, alivuliwa wadhifa wake siku moja baada ya kupokea ripoti ya Kamati ya uchunguzi juu ya tukio uvamizi wa kituo cha televisheni cha Clouds.

Ripoti ya kamati aliyoiunda Nape kuchunguza tukio hilo, ilithibitisha kuvamia kituo hicho Machi 17, 2017 na alifanya uvamizi huo akitumia askari wenye silaha.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,407FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles