26.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 7, 2021

Wafanyabiashara walalamikia taasisi za Serikali

Na OSCAR ASSENGA-TANGA

JUMUIYA za wafanyabiashara wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, wameitaka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kudhibiti urasimu unaosababishwa na taasisi za ukaguzi wa bidhaa ili kuwavutia wafanyabiashara wa ndani.

Hayo yamesemwa jana kwenye mkutano maalumu wa jumuiya hizo walipokutana na maofisa kutoka taasisi mbalimbali kwa lengo la kuwashawishi wafanyabiashara hao, waanze kuitumia Bandari ya Tanga kuingiza na kusafirisha bidhaa zao.

Mkurugenzi wa kiwanda cha Jayjey Ltd cha mjini Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro, Humphrey Mosha, alisema ili kuzinusuru bandari za ndani ya nchi, kuna haja ya kuwekwa mikakati ya kukabiliana na watu wanaorudisha nyuma biashara bandarini zikiwamo taasisi hizo za ukaguzi.

“Taasisi kama TBS, TFDA, TRA na Mkemia Mkuu wa Serikali, zinasababisha baadhi ya wafanyabiashara hasa wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini, kutumia Bandari ya Mombasa nchini Kenya, kwa kuwa huko hakuna usumbufu kama wa Tanzania.

“Niliwahi kutumia Bandari ya Dar es Salaam zaidi ya mara tatu, lakini kutokana na tabia zao mbovu na urasimu kwa taasisi hizo, ghafla nikahamia Bandari ya Mombasa na sikufikiria Bandari ya Tanga.

“Kwa hiyo, hizo taasisi zisipodhibitiwa nawaambia lazima bandari zetu zitakufa kwa sababu kuna usumbufu usiokuwa na maana,” alisema Mosha.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Shirima, alisema matatizo yaliyopo katika bandari za ndani ni pamoja na ucheleweshwaji wa mizigo na urasimu kwa watumishi na taasisi zilizo na mamlaka.

Awali, akizungumzia maboresho ya bandari hiyo, Meneja wa Bandari ya Tanga, Percival Salama, alisema kuna maboresho makubwa yamefanyika ili kutengeneza mazingira rafiki kwa wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na upakiaji na upakuaji wa mizigo ambao hauzidi siku nne.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,400FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles