24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Zahera atamba Yanga itaimaliza Pyramids leo Kirumba

MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM

WAWAKILISHI pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga leo watakuwa kibarua kigumu cha kusaka ushindi dhidi ya timu ya  Pyramids ya Misri, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, utakaochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Yanga itatakiwa kupata ushindi mnono katika mchezo huo wa nyumbani ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kusonga mbele kabla ya mchezo wa marudiano utakaochezwa  Novemba 3, mwaka huu Uwanja wa June 30, Cairo.

Yanga iliangukia Kombe la Shirikisho, baada ya kuondolewa Ligi ya Mabingwa Afrika na Zesco United  ya Zambia,  kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2. 

Pyramids kwa upande wake, iliiondosha mashindanoni Etoile Du Congo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC), kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-1, zilipokutana raundi ya awali kabla ya kutinga raundi ya kwanza na kuitimua CR Belouizdad ya Algeria kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1.

Mara ya mwisho Yanga kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika  ilikuwa mwaka 2017,  baada ya kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 2-1 dhidi ya Wolayta Dichaa ya Ethiopia.

Pyramids inashiriki michuano hiyo kwa mara kwanza. Ilikata tiketi hiyo  baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Misri,   nyuma ya mabingwa Al Alhly na Zamalek iliyomaliza nafasi ya pili.

 

Licha ya uchanga ilionao,  Pyramids inajivunia uwekezaji mkubwa ilioufanya katika kikosi chake kwani imesajiliwa wachezaji wenye ubora mkubwa.

 

Inatwajwa kuwa thamani ya Sh Bilioni 52. 2, fedha iliyowekezwa na Bilionea  Salem Al Shamsi .

Shamsi aliinunua klabu hiyo Juni mwaka huu.

 

Pyrmids ilianzishwa miaka 12 iliyopita ikianza kuitwa Al Assiouty Sport, kabla ya kubadilishwa jina mwaka jana na  kuitwa Pyramid FC,  baada ya kununuliwa na bilionea, Turk Al Sheikh raia wa Saudia.

 

Ilianza kushiriki kushiriki Ligi Kuu Misri mwaka 2014, lakini mafanikio makubwa zaidi iliyopata msimu uliopita,  baada ya kumaliza nafasi ya tatu, huku ikipoteza michezo miwili pekee.

 

Hata hivyo, Yanga itaingia katika mchezo huo ikijivunia rekodi ya nzuri ya kucheza michezo mitatu  ya  mwisho ya kimataifa Uwanja wa Kirumba bila kupoteza.

Yanga ilianza kukutana na Mamelody Sundowns ya Afrika Kusini, hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mchezo uliochezwa mwaka 2001 na kumalizika kwa sare ya mabao 3-3.

Mwaka 2007, Yanga iliumana na Esperance ya Tunisia, mchezo wa hatua 16 bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika na kutoka suluhu.

Suluhu hiyo iliifanya Yanta kutupwa nje ya michuano hiyo na kuangukia hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho.

Huko ilikutana na El Maerreikh ya Sudan na matokeo ya mchezo kuwa suluhu.

Rekodi zinaonyesha, miaka ya karibuni Yanga imekuwa ikipata matokeo mazuri inapocheza nyumbani dhidi ya timu kutoka Misri.

Mwaka 2014 iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Alhly, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga leo itawakosa nyota wake watatu, beki kisiki Lamine Moro ambaye anatumia adhabu ya kadi nyekundi aliyopewa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Zesco, Maybin Kalengo na Sadney Urikhob wanaosumbuliwa na majeraha.

Kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera alisema amejigamba kuwa yuko tayari kuwakabili waarabu hao na kuwashinda.

“Tumewaona wapinzani wangu Pyramids kwa kupitia video na marafiki zangu wa karibu, ni wazuri kwenye mipira mirefu ya kushambulia kwa kushtukiza.

“Tayari nimewapa mbinu mabeki wangu jinsi ya kucheza mipira hiyo na kikubwa tutakachokifanya ni kuzuia njia zao wanazozitumia katika kushambulia goli letu,”alisema Zahera.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles