Marekani yamwekea vikwazo waziri wa ulinzi wa Zimbabwe

0
569

HARARE, ZIMBABWE

WAKATI nchi za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika zikiendelea kupaza sauti zikitaka nchi ya Zimbabwe iondolewe vikwazo, Marekani imesema haitomruhusu Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo, Owen Ncube kuingia nchini humo.

Imesema hatua hiyo inatokana na Serikali ya nchi hiyo kuvunja maandamano yaliyofanywa na waandamanaji, asasi za kiraia na upinzani.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema haitampatia hati ya kuingia nchini humo waziri huyo chini ya sheria ya vikwazo kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki.

Akizungumzia uamuzi huo Waziri wa Mambo Nje wa Marekani, Mike Pompeo ameitaka serikali ya Zimbabwe kutuliza ghasia, kufanya uchunguzi na kuwawajibisha maofisa waliohusika na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Kauli ya Marekani imetolewa muda mfupi baada ya serikali ya Rais Emerson Mnangagwa nayo kuratibu maandamano mjini Harare kutaka nchi hiyo iondolewe vikwazo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here