23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

Madrid yamweka Bale chambo kumpata Pogba

MADRID, HISPANIA

KOCHA wa Real Madrid Zinedine Zidane yuko tayari kuhakikisha klabu hiyo inainasa saini ya Paul Pogba na anaweza kutoa pauni milioni 85 pamoja na Gareth Bale  ili kufanikisha dili hilo, kulingana na ripoti kutoka Eldesmarque.

Zidane amekuwa akitafuta njia ya kumwachia Bale aondoke tangu alipochukua kibarua hicho na amekuwa akitamani kumsaini Pogba.

Madrid haikuweza kufikia dau la Pauni Milioni 180  lililowekwa na klabu yake ya Manchester United ili kumuachia katika dirisha la usajili lililopita.

Mabingwa hao wa zamani wa Ulaya walitumia kitita cha zaidi ya pauni milioni 300 katika dirisha lililopita, lakini Zidane bado alikuwa akimtaka Pogba kama kipaumbele chake cha  kwanza.

Pogba  kwa sasa anaendelea kuuguza majeraha ya kifundo cha mguu (ankle)  na hakusafiri kwenda Belgrade kwa mechi ya Ligi ya Europa League katikati mwa wiki.

Kiungo huyo raia wa Ufaransa alitumia wakati mwingi huko Dubai akifanya mazoezi ya hali ya hewa ya joto wakati wa mapumziko ya kimataifa kujaribu kupata tena usawa, lakini hakupona kwa wakati.

Kuongeza zaidi kwa uvumi wa uhamisho  wa hivi karibuni, kulichangiwa na tetesi za Pogba kuonekana akikutana na Zidane alipokuwa Dubai.

Katika miezi michache iliyopita, Pogba ametoa siri ndogo ya kutamani kuichezea Madrid, akikubali mara kadhaa kwamba Zidane alikuwa mfano wake kama kijana.

Bale amepata nafasi ya kudumu kwenye timu ya kuanza kwa Real Madrid lakini amefanikiwa kufunga mabao mawili hadi sasa msimu huu, na kuongeza kwa mkanganyiko wa Zidane.

Bale alikaribia kutua China katika dirisha lililopita , lakini mpango huo ulizimwa na Rais wa klabu hiyo, Florentino Perez.

Inaonekana Perez yuko tayari katika mpango huo wa kukadilishana ambao uanweza kumshawishi Ole Gunnar Solskjaer na United kumruhusu Pogba ambaye mkataba wake na klabu hiyo unamalizika 2021.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles