24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Watu zaidi ya 400 kuhudhuria Siku ya Makumbusho

Ferdnanda Mbamila, Dar es Salaam

Watu  zaidi ya 400 wanatarajia kuhudhuria katika sikukuu ya  Makumbusho duniani(IMD),yatakayofanyika  katika Kijiji cha Makumbusho , jijini Dar es Salaam.

Maadhimisho ya sikukuu hiyo hufanyika  Mei 18 kila mwaka, huadhimishwa kwa kaulimbiu tofauti ambapo kwa mwaka huu kaulimbiu inasema  “makumbusho  kitovu cha utamaduni”.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Mei 16, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Profesa Audax Mabula amesema lengo la kuwa makumbusho duniani ni kuleta uelewa  kwa umma kwamba makumbusho ni taasisi ambayo urithi wa utamaduni unahifadhiwa   na utamaduni ni uhai wa nchi.

Amesema utamaduni ulio hai unabadilishana , unahuishwa na kurutubishwa  na hivyo kuwa maelewano,ushirikiano na amani miongoni mwa wananchi.

“Kama taasisi za makumbusho zina  nguvu na uwezo wa kuleta utengamano wa kiutamaduni  na kisiasa  na kujenga umoja wa kitaifa,uzalendo  na kuwafanya watu wathamini na kuhifadhi urithi wa  utamaduni na asili kwa  kizazi hiki na kijacho,”amesema.

Amesema makumbusho  zinaendelea kufanya kazi  zake  za misingi  za utafiti, uhifadhi, kukusanya mikusanyiko na kuelimisha umma kwa njia ya maonesho, semina, machapisho na program za kielimu juu ya mambo yote yanayohusu urithi wa asili  na kiutamaduni kwa lengo la kutoa elimu, kujifunza na kuburudisha.

Amesema kwa sasa makumbusho  duniani kote  zina jukumu kubwa la kuihudumia jamii kuifanya kuufikia urithi wao  wa utamaduni na asili.

Profesa Mabula amesema pia katika kuadhimisha  siku hiyo makumbusho ya taifa imeandaa tamasha la mama na mwana ambalo litahusisha  wazazi na watoto wao kutembelea makumbusho na kujifunza juu ya urithi  wao.

“Tamasha la Mama na Mwana litajumuisha mambo yafuatayo, maandamano yatakayoanzia eneo la bamaga au  kwenda kijiji cha makumbusho na maeneo mengine.

“Watoto na wazazi wao  kucheza michezo mbali mbali ya asili, kujifunza kupika vyakula vya asili, kuruka kamba ,mdako, kombolela, kidalipo, , kuchora na michezo mingine mingi,”amesema Profesa Mabula.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles