27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge aeleza sababu za kuangua kilio bungeni

Arodia Peter, Dodoma

Mbunge  wa Mlimba, Suzan Kiwanga (Chadema), ameeleza sababu za kuangua kilio bungeni wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kuwa ni kutokana na adha ya ubovu uliokithiri wa barabara ya Mlimba hadi mpakani mwa Mkoa wa Njombe eneo la Lwamote.

Akizungumza na Mtanzania Digital katika viwanja vya Bunge leo Mei 16,  Kiwanga amesema hali katika barabara hiyo ni mbaya na katika kipindi hiki cha mvua mabasi ya abiria yanayojaribu kwenda kule yanakaa njiani zaidi ya siku tatu huku abiria wengine wakiwa ni wagonjwa, watoto na wazee.

 “Hivi ninavyoongea hata kijiko kilichokwenda kukwamua magari yaliyokwama na kusawazisha baadhi ya maeneo kwenye barabara hiyo kimezama kabisa, kuna basi lilikwama kwa siku tatu, wananchi wanataabika, nilipokumbuka adha hizo nilijikuta ninatoa machozi.

 “Kuna hatari watu wengine wanaweza kupata magonjwa ya mshtuko kama presha na hata kufia njiani kwa sababu kama kijiko (katapila) kinazama unategemea nini kwa mabasi ya kawaida?,” alihoji Kiwanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles