23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wafamasia watakiwa kuwa na orodha ya dawa

RAMADHAN HASSAN-DODOMA

SERIKALI imewataka wafamasia wote nchini kuhakikisha wanakuwa na orodha ya dawa zinazoingia katika vituo vyao na jinsi zilivyotumika ili kuziba mianya ya wizi wa dawa maeneo yao.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini hapa na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia afya, Ofisi ya Rais Tamisemi, Dk. Dorothy Gwajima wakati akizungumza katika kikao kazi cha wafamasia wa mikoa yote nchini.

Dk. Gwajima alisema kumekuwa na wizi mkubwa wa dawa katika vituo vya afya hali inayowanyima usingizi kwa kuwa kila siku kwenye vyombo vya habari wanaripoti wizi wa dawa nchini.

“Halafu wanaofanya huo wizi mnawajua kwa kuwa mko nao kila siku, kwa sababu kama mngekuwa hamuwajui msingewataja mnapobananishwa, kwanini msiwataje kabla hamjabananishwa, mnasubiri mpaka wakaguzi waje ndiyo mnaanza kutaja.

“Hakikisheni kila dawa inayoingia mnaiwekea rekodi na pia inapotoka ili kujiridhisha matumizi ya dawa zinazoingia na matumizi yake, siyo kila wiki mtu anakuja kuomba kopo la dawa ya Paracetamol ambalo wanapaswa kutumia watu 90 yeye anatumia kwa wiki moja, aonyeshe matumizi ya hizo dawa maana hawa wezi wana mbinu nyingi wanazozitumia ili kufanikisha wizi wao,” alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Afya Tamisemi, Dk. Ntuli Kapologwe alisema upatikanaji wa dawa katika sekta ya afya ni eneo muhimu sana, hivyo kila mtoa huduma ni lazima ahakikishe kuwa wagonjwa wote wanaofika katika kituo chake kupata huduma wapewe dawa kulingana na mahitaji yao.

Alisema bila ya kuwa na dawa majengo yote ya vituo vya afya, zahanati na hospitali zinazojengwa na Serikali yatakuwa hayana maana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles