24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Samatta bado aiota VAR

GENK, UBELGIJI

NAHODHA wa timu ya K.R.C Genk ya nchini Ubelgiji, Mbwana Samatta ambaye pia ni nahodha wa timu ya Taifa Tanzanian ‘Taifa Stars’ amedai hana bahati na mfumo wa VAR.

K.R.C Genk wiki moja iliopita ilishuka dimbani kwenye uwanja wa nyumbani dhidi ya wapinzani wao Liverpool kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya huku K.R.C Genk ikikubali kichapo cha mabao 4-1.

Samatta alifanikiwa kupachikanbao, lakini lilikataliwa na mfumo wa VAR huku ikidaiwa Junya Ito ambaye alipiga pasi ya mwisho alikuwa kwenye eneo la kuotea.

Samatta amedai anajiona mtu ambaye hana bahati na mfumo wa VAR ikiwa hadi sasa jumla ya mabao yake matatu yamekataliwa kwenye michezo mbalimbali.

“Hilo lilikuwa bao langu la tatu ambalo limekataliwa na mfumo wa VAR msimu huu, ukweli ni kwamba nilikuwa na furaha kubwa kufunga bao dhidi ya moja kati ya timu kubwa duniani, lakini mwisho wa siku halikukubaliwa.

“Wakati mchezo umesimama kupisha VAR ifanye maamuzi nilikuwa nafanya maombi ili likubaliwe kwa kuwa niliamini ni jambo la kihistoria katika maisha yangu yote ya soka.

“Lakini ukweli ni kwamba nitaendelea kulikumbuka bao hilo, hata kama halikukubaliwa nitaendelea kuliweka kwenye kichwa changu kwa kuwa nilifunga dhidi ya Liverpool na likakataliwa.” Alisema Samatta.

Samatta aliongeza kwa kusema, mchezo wa marudiano dhidi ya Liverpool kwenye uwanja wa Anfi eld utakuwa mgumu, huku klabu yake hadi sasa ikiwa haijafanikiwa kupata ushindi katika hatua hiyo ya makundi.

“Niwe mkweli, mchezo kwenye uwanja wa Anfi eld utakuwa mgumu sana kwa kuwa wao hawatokuwa tayari kuupoteza mchezo huo kwenye uwanja wa nyumbani dhidi ya idadi kubwa ya mashabiki huku sisi tukipambana kutafuta ushindi wetu wa kwanza,” aliongeza mchezaji huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles