24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

UVCCM YAHAMASISHA VIJANA KUJIUNGA NSSF, NHIF

MWANDISHI WETU -SONGWE


MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Songwe, Andrew Kadege, amewataka vijana kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),  kunufaika na huduma zinazotolewa na taasisi hizo.

Kadege alitoa rai hiyo jana wakati alipokutana na viongozi wa waendesha bajaj na pikipiki   wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma.

“Nchi yetu inaongozwa kwa mujibu wa sheria na katiba, hakuna yeyote aliye juu ya sheria, hivyo ninaomba viongozi wenzangu wa bajaj na bodaboda tukawe mabalozi kwa wanachama wenzetu kwamba ni lazima tutii sheria kwanza kabla ya kuanza kudai haki.

“Ni muhimu sasa tukawa na uongozi rasmi unaotambulika na wenye katiba  muweze kunufaika na mambo mbalimbali kutoka serikalini na kwenye jamii.

“Lakini pia mnatakiwa kuwa wazalendo kwa nchi na kuilinda kama ulinzi shirikishi katika mapambano ya usafirishaji binadamu, biashara za magendo na biashara nyingine haramu,” alisema Kadege.

Alilionya jeshi la polisi kujichukulia sheria mkononi hasa kwa kuwachapa viboko waendesha bodaboda wakati wa usiku kama walivyolalamika viongozi hao.

Kadege aliiomba Halmashauri ya Mji wa Tunduma kupitia Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura), kuikarabati barabara mchepusho maarufu kama barabara ya zamani ili kupunguza foleni kwenye barabara kubwa inayoenda Zambia.

Meneja wa NHIF Mkoa wa Songwe, Simon Mmbaga, alisema mfuko ulianzishwa  kusimamia upatikanaji wa huduma za matibabu kwa watumishi wa umma, binafsi, wanafunzi na makundi mbalimbali ya watu ili kupata huduma za matibabu kupitia vya afya vya serikali.

Alisema kwa sababu hiyo  madereva bajaj na bodaboda ni walengwa na wana sifa zote za kujiunga kama wanachama wa vikundi vya ujasiriamali vilivyosajiliwa.

Mwakilishi wa NSSF, Khadija Hassan alisema  mtu binafsi aliyejiajiri na vikundi vilivyoanzishwa katika sekta isiyo rasmi mfano bodaboda na bajaj wanaweza kujiunga na mfuko huo.

Alisema ili kuwa mwanachama kiwango cha chini cha kuchangia ni Sh 20,000 kwa mwezi na wananchama wanaweza kupata matibabu kwa kituo atakachochagua  zaidi ya 177  ndani ya Mkoa wa Songwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles