23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

DC AFUNGA MGODI WA DHAHABU KIBAGA

Na TIMOTHY ITEMBE – TARIME


MKUU wa Wilaya Tarime, Glorius Luoga ameufunga kwa muda usiojulikana Mgodi wa Dhahabu wa Kibaga  katika Kijiji cha Kebaga Kata ya Kenyamanyori   kwa madai ya kutozingatia masharti ya uchimbaji madini   nchini.

Akifunga mgodi huo juzi, Luoga alisema  amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa wananchi mbalimbali kuwa wachimbaji wa mgodi huo wanaendesha shuguli hizo kinyume cha utaratibu bila kuzingatia masharti ya uchimbaji ikiwa ni pamoja na kuwanyanyasa wafanyakazi.

“Mgodi huu una shida ya kulipa ushuru kwa halmashauri bado hawajalipa, lakini wao wenyewe wanagombana kutokana na kukosa utaratibu  mzuri wa kugawana mawe yanayotoka ndani ya mgodi.

“Sasa wakae watatue matatizo haya ili wenye mashimo wapate haki yao, wenye viwanja na hata wale wenye milipuko,” alisema.

Alisema amesimamisha uzalishaji wa mgodi huo na kuacha kazi ya kina mama ambao wamekuwa wakiokota mabaki ya mawe.

Alionya  kuwa kuanzia sasa hawataruhusiwa kuingia ndani ya shimo hadi watakapokubaliana na kufuata taratibu nzuri na kurejea kwake kumueleza wamekubaliana ikiwa ni pamoja na kulipia ushuru wa halmashauri.

Kamishna Masaidizi wa Madini Mkoa Mara, Nyaisaro Mugaya, alisema alikuwa akitembelea wachimbaji hao kwa muda ikiwamo kukaa nao mara kadhaa kwa kuwataka kutatua mgogoro wao ambao ulikuwa ukihatarisha amani lakini hali hiyo ilishindikana.

Mugaya alisema alifika mara kwa mara na kujadiliana nao lakini bado walishindwa kuzingatia makubaliano ambayo walikubaliana.

Alisema  kila alipoondoka   waliendelea na mambo yao hivyo kuendelea kwa mgogoro.

Katika hatua nyingine, Septemba 20, mwaka huu Diwani Kata ya Kenyamanyori, Ganga Mugendi (CCM) Halmashauri ya Mji wa Tarime alivamiwa na kukatwa mapanga   kichwani.

Alilazwa katika Hospitali ya Bomani baadaye kuhamishiwa Bugando,  Mwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles