Imechapishwa: Fri, Sep 1st, 2017

UCHAGUZI KENYA KURUDIWA NDANI YA SIKU 60

Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Kenya yameingia shubiri baada ya Mahakama Kuu nchini humo, kubatilisha ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta dhidi ya mpinzani wake mkuu Raila Odinga na kuamuru uchaguzi huo urudiwe ndani ya siku 60.

Uamuzi huo umefikiwa leo Septemba 1, kutokana na maombi ya Odinga ambaye ni mgombea wa Muungano wa Upinzani NASA, ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti 8, mwaka huu, uliompa ushindi Rais Kenyatta.

Katika maombi yake, Odinga alisema kura zake zilipunguzwa kwenye baadhi ya vituo na kuongezewa mpinzani wake, lakini kubwa zaidi ni kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi ambapo baadhi ya fomu muhimu za matokeo ya uchaguzi kama vile fomu namba 34A, B na C, hazikupatikana siku ya kutangazwa kwa matokeo.

Katika shauri hilo, majaji wanne kati ya sita, wamekubaliana kuwa Tume Huru ya Uchaguzi  (IEBC), imeshindwa kusimamia vema uchaguzi huo na hivyo kusababisha kasoro kadhaa kwenda kinyume na katiba ya Kenya.

Pamoja na mambo mengine, akizungumza baada ya uamuzi huo wa mahakama Odinga amesema NASA itawashtaki maofisa wa tume kwa kufanya uhalifu mkubwa kwa nchi hiyo.

Baada ya uamuzi huo kutolewa, baadhi ya wafuasi wa Odinga walionekana kufurahi kwa kuimba mapambio huku wale wa Kenyatta wakizimia na wengine kuongea kwa hasira kama ishara ya kupinga uamuzi huo wa mahakama.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

UCHAGUZI KENYA KURUDIWA NDANI YA SIKU 60