28.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

MEYA ARUSHA AMJARIBU RC GAMBO

Na JANETH MUSHI-ARUSHA

MEYA wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Calist Lazaro (Chadema), amemvaa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo  na kudai kwamba ameshindwa kuheshimu viongozi wenzake kutokana na kutojua kuongoza kwa kufuata msingi ya utawala bora.

Pamoja na hali hiyo alimtaka Gambo kuacha kuingiza siasa katika kutatua masuala mbalimbali ikiwamo migogoro ya ardhi ambayo inatakiwa kutatuliwa kisheria kwa kufuata ngazi za utawala.

Akizungumzia na waandishi wa habari jana jijini hapa, Meya Lazaro, alisema ziara za mkuu huyo wa mkoa zitaendelea kuchochea migogoro ya ardhi badala ya kupunguza.

“Gambo anaingilia majukumu yasiyomhusu anaita wananchi kusikiliza kero za migogoro ya ardhi inayowakabili, wakati migogoro ipo kwenye mabaraza ya ardhi ya kata, wilaya na nyingine mahakamani kitengo cha ardhi.

“Hajui taratibu, sheria, utawala bora na haheshimu viongozi wenzake, amekuja ofisi za Jiji kusikiliza kero za wananchi lakini hakushirikisha viongozi wa halmashauri alipaswa kuelewa taratibu kwani migogoro inasikilizwa kwenye mabaraza na anajua kwamba Jeshi la Polisi haliwezi kutatua migogoro ya ardhi,” alisema Lazaro

Meya huyo alilaaini kitendo hicho kilichokwenda pamoja na kutesa watumishi wa jiji hilo kwa siku mbili kutokana na kulazimika kukaa maofisini mwao hadi saa saba za usiku ili kumsikiliza Gambo aliyejigeuza diwani, mbunge na afisa ardhi wa Arusha.

“Juzi na jana shughuli za Jiji zilisimama kwa sababu ya ziara ya Gambo, naomba ieleweke sina shida na yeye kutembelea halmashauri au kutatua kero eneo la utawala wake, nina tatizo kwenye maeneo mawili hajui utawala bora au utawala wa kisheria,” alisema.

Alidai kiongozi huyo ameacha kero za msingi zilizowasilishwa Kamati ya Ulinzi na usalama kuhusu mgogoro wa Shule ya Msingi Naura na Jeshi la Polisi ambapo magari yenye makosa yanayokamatwa yamekuwa yakiegeshwa eneo la shule hiyo.

MTANZANIA lililopomtafuta Gambo ili kutoa ufafanuzi wa madai hayo hakuwezi kupokea simu ambapo baada ya muda simu yake ilituma ujumbe mfupi wa maandishi uliosomeka; “Samahani ndugu yangu, nipo kikaoni nitarudi kwako nikimaliza! Mrisho Gambo,” aliandika Gambo ujumbe mfupi kwa njia ya simu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles