23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Tanga yapata vituo vitano vya upasuaji wa dharura

Na Amina Omari,Tanga

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema kwa mara ya kwanza Jiji la Tanga limeweza kupata vituo vitano vya afya vyenye huduma ya upasuaji wa dharura.

Ameyasema hayo leo Jumapili Julai 7, wakati Mwenge wa Uhuru ulipopita katika kuzindua mradi wa upanuzi wa kituo cha afya cha Duga.

Amesema kuwa ndani ya miaka mitatu ya Rais John Magufuli, jiji hilo limeweza kujengewa vituo vinne na kufanya kuwa na jumla ya vituo vitano vyenye huduma ya dharura ya upasuaji.

Amesema kuwa kwa mara ya kwanza kwa uwepo wa vituo hivyo jiji la Tanga litaweza kufanya upasuaji wa dharura kwa mama wajawazito bila ya kulazimika kuifuata huduma hiyo katika hospitali ya Rufaa ya Bombo.

“Tunashukuru Rais Magufuli ameweza kuokoa wajawazito na kuepusha vifo vya watoto wachanga katika Jiji la Tanga, kwa kuhakikisha anawaboreshea huduma za mama na mtoto,”amesema Waziri Ummy.

Naye Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa, Mzee Mkongea Ally, ameitaka Halmashauri ya Jiji la Tanga kuhakikisha wanamaliza ujenzi wa miundombinu katika kituo hicho ili wananchi waweze kupata huduma ya haraka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles