22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Wajawazito watakiwa kuacha kutumia mitishamba kuvuta uchungu

Na Amina Omari,Tanga

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa, Mzee Mkongea Ally, amewataka wajawazito kuacha kutumia dawa za mitishamba kuvuta uchungu badala yake waende hospitali ili kupata huduma bora za afya.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumapili Julai 7,  wakati Mwenge wa Uhuru ulipopita kukagua mradi wa kituo cha afya cha Ngamiani

Amesema kuwa lengo la Serikali kuboresha huduma za afya ni kuhakikisha wananchi wote wapata huduma za afya zilizobora.

“Kina mama wajawazito tuache kutumia dawa za kienyeji na mitishamba badala yake tumieni vituo vya Afya vilivyoboreshwa kwa ajili yakupata huduma bora,” amesema Ally.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa, amesema kuwa mradi huo umegharimu kiasi cha Sh. milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa miundombinu ya kituo hicho.

Amesema kuwa kukamilika kwa kituo hicho kutatoa fursa ya wananchi wengi kupata huduma za kimatibabu na kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya Rufaa ya Bombo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles