25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

TAMASHA NA MIKAKATI ZAIDI NDANI YA UKATILI WA KIJINSIA

Na Elias Simon, Dar es salaam

Taasisi ya maendeleo shirikishi kwa vijana (TAMASHA) Leo tarehe 28November imeendelea kuweka mikakati juu ya vijana kupitia upande wa harakati juu ya kuzuia ukatili wa kijinsia kwa upande wanawake ambapo imelenga kuonesha kupinga vikali ukatili wa kijinsia.

Akizungumza kwenye mahojiano na Mwandishi wa habari, mratibu wa TAMASHA bwan. Geeorge mwita amesema katika kuunga mkono wiki hii ya ukatili wa kijinsia kwa siku hizi kumi na sita 16, wamelenga kuonesha madhara ya kijinsia yanayoendelea kwa wamama na wasichana .

“Sisi kama TAMASHA tumejipanga kuandaa taarifa za jumbe mbalimbali kupitia kupinga vikali ukatill huu wa kijinsia  kwa kuunga mkono harakati kwa mfano matangazo kwenye mitandano ya kijamii yetu na  kupitia mashuleni kwa kuelezea ukatili wa kijinsia ni nini? Na pia Kkwa kufanya vipindi” Alisema Mratibu Dedi. Akiongezea mengine kwa upande wa kazi zingine za TAMASHA kwa sasa wao kama Taasisi  wanaendeleza nguvu kazi zao watazoenda kuzifanya katika kijiji cha Mbasemi, wilaya ya Meru, mkoani Arusha, ndani ya tarehe 7 Disemba hadi  28 Disemba ambapo ni mara ya pili kuweka kambi katika kijiji hicho kwa kufanya shughuli za kijamii kama kujenga ofisi za seriakali za mitaa, kukarabati barabara, kufanya michango, pia kutoa misaada kwa wasiojiweza

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles