Mfumo wa vifurushi vya bima ya afya yazinduliwa rasmi

0
915

Aveline Kitomary, Dar es salaam

Mfumo wa Taifa wa vifurushi vya bima ya afya umezinduliwa rasmi leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ambao unavifurushi vitatu vya Jali, Timiza na wekeza afya.

Akizungumza Kwa niaba ya Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Ummy Mwalimu, Mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa bima ya Taifa (NHIF), Anna Makinda, amesema vifurushi hivyo vitasaidia wananchi hasa wenye kipato cha chini kupata huduma bora za katibu katika hospitali yoyote nchini.

“Wakati huu sasa ni wa mashindano watakaotoa huduma nzuri ndio watapata fedha nyingi hivyo wahudumu wa afya wanatakiwa wafanyakazi kwa bidii na pia huduma za hospitali ziboreshwe kwani mfumo huu wa bima pia utahusu hospitali za binafsi.

“Nina imani kubwa kuwa mfumo huu wa bima utasaidia wananchi wengi kupata huduma za afya hasa walio na uwezo mdogo,bodaboda na wamachinga watakuwa wanafika wakubwa wa vifurushi hivi,”amesema Makinda.

Pia amesema wahudumu wa afya sasa watapita katika kila mtaa ili kutoa elimu kuhusu vifurushi hivyo ili kuwavutia Wananchi anaendelea kujiunga na mfumo huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here