SPIKA NDUGAI ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MAPACHA WALIOUNGANA

0
105

Elizabeth Hombo, Dodoma


Spika wa Bunge, Job Ndugai ametuma salamu za pole kwa familia ya Maria na Consolata Mwakikuti, waliofariki dunia juzi usiku, katika Hospitali ya Mkoa ya Iringa.

Spika Ndugai ametoa salamu hizo leo bungeni jijini Dodoma, muda mfupi baada kumalizika kipindi cha maswali na majibu.

“Natoa salamu za rambirambi kwa familia ya watoto hawa Maria na Consolata na mazishi yao inaweza kuwa leo huko Iringa.

“Walikuwa watoto wenye upendo sana. Kifo chao ni wazi kimetuumiza sote.

“Waziri wa Elimu (Profesa Joyce Ndalichako) tufikishie pole zetu huko,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here