30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

USAFIRI WA MWENDOKASI KUSUKWA UPYA (1)

Na Bakari Kimwanga-DAR ES SALAAM


WAKATI wananchi wanaopata huduma za usafiri wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam wakilalamikia ubora wa huduma hiyo, Serikali kupitia Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), imesema ipo mbioni kupata mwekezaji mwingine atakayeendesha mradi huo.

Mwekezaji huyo atakuja na mabasi 305 ambayo yatatoa huduma kwenye barabara zote za mradi na njia mlisho (njia za pembezoni) zilizo nje ya mradi.

Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi wanaotumia huduma hiyo kulalamikia uchache wa mabasi, hali inayowafanya wakae vituoni kwa zaidi ya saa tatu kusubiri usafiri huo, hasa asubuhi wanapokuwa wanakwenda kwenye shughuli zao na jioni wakati wa kurudi.

Uchunguzi uliofanywa na MTANZANIA kwa zaidi ya miezi miwili katika maeneo mbalimbali ambayo usafiri huo unapatikana, madudu kadhaa yamebainika ikiwamo ubovu wa mabasi, changamoto kwenye tiketi na wananchi kukaa muda mrefu vituoni kusubiri huduma hiyo.

Changamoto nyingine ni pamoja na kile kinachoonekana kwa mwendeshaji kushindwa kujua ubovu wa mabasi hayo na kuwapo matairi vipara jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa abiria.

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya mabasi yamekuwa yakizima katikati ya barabara na kulazimika mabasi hayo kuhama kwenye barabara yake na kutumia njia za kawaida kwa kuchanganyika na magari mengine.

Kwa habari zaidi pata nakala yako ya gazeti la MTANZANIA hapo juu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles