24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yakanusha uwepo wa ebola nchini

Na AVELINE KITOMARY, DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amekanusha tetesi za kuwepo kwa ugonjwa wa ebola nchini na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari zaidi dhidi ya ugonjwa huo.

Ummya alisema kuwa awali watu wawili walikuwa wakishukiwa kuwa na ugonjwa huo lakini baada ya vipimo, walijiridhisha walibainika hawana virusi hivyo.

Awali taarifa zilisambaa katika mitandao ya kijamii ikionesha Shirika la Afya Duniani  (WHO) limetoa tahadhari yam to mmoja kuwa amefariki nchini kwasababu ya ugonjwa ambao haujajulikana.

Baadaye Ubalozi wa Marekani nchini pia ulirejea taarifa hiyo ya WHO huku ikiahidi raia wake kuwa itaendelea kutoa taarifa zaidi kadri zitakavyopatikana.

Pia taarifa nyingine za kwenye mitandao ya kijamii, zilidai mwanamke mwenye umri miaka 36 aliyekuwa akisoma nchini Uganda, alifariki akiwa katika Jiji la Dar es salaam kwa ugonjwa ambao haujajulikana na akazikwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es salaam jana, Ummya alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea kuchukua tahadhari kutokana na ugonjwa huo kuwepo nchi za jirani za DRC Kongo na Uganda.

“Tumekuja kutoa ufafanuzi kuhusu uvumi unaosambaa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari ukisema hapa nchini kuna ugonjwa wa ebola, Wizara inawasihi wananchi kutokuwa na hofu kwani mpaka sasa hakuna mtu aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa huo.

“Kwa mujibu wa sheria ya afya namba moja ya mwaka 2009, mwenye dhamana ya kutoa taarifa ya magonjwa ya mlipuko ikiwamo ebola ni waziri mwenye dhamana na masuala ya afya, hivyo kutoa taarifa bila mamlaka husika ni kosa kisheria.

“Tumeimarisha uratibu na ufuatiliaji wa ugonjwa huu tangu ulipotangazwa, tumeweka mikakati mbalimbali ili kuhakikisha ugonjwa huu hauingii nchini na tunaendelea kuchukua tahadhara zaidi,”alisema Ummy.

HATUA ZA UDHIBITI

Ummy alisema katika kudhibiti ugonjwa huo, wanaendele …

Habari kamili jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles