25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Baadhi ya wenye visima wanakunywa maji ya chooni – Mkemia Mkuu

Na Hamisa Maganga-Dar es Salaam

MENEJA wa Maabara ya Maikrobailojia kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Faustine Wanjala, amesema watu wanaotumia maji ya visima bila kuyapima, wanauwezekano mkubwa wa kunywa maji ya chooni yanayotoka kwa majirani zao.

Akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa kupima sampuli za vinywaji, chakula, dawa, mazao na bidhaa zake, wakati wa mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari, Dar es Salaam juzi, Wanjala alisema wapo watu ambao wanakunywa maji ya chooni bila wao kujua. 

Alisema asilimia kubwa ya watu wanaochimba visima vya maji majumbani kwao kwa ajili ya matumizi ya kupikia na kunywa, wengi hawana utaratibu wa kuyapima kujua kama ni salama au laa.

“Utakuta mtu amechimba kisima nyumbani kwake anaona kila siku kinajaa maji hayakauki, akiangalia nyumba ya pili jirani yake naye ana kisima lakini hakina maji anaanza kumcheka kwamba kisima chake hakina maji, hajiulizi ya kwake yanatoka wapi.

“Kila siku kisima kimejaa, iwe jua iwe mvua hakikauki, kumbe maji yanayojaa yanatoka kwenye choo cha jirani yake, yeye hajui anatumia tu.

“Jirani anaingia chooni anaoga, anajisaidia na yale maji anayoyatumia yote yanatiririka yanakwenda kujaa kwenye kisima chake bila yeye kujua,” alisema Wanjala.

Alisema kutokana na maji hayo, kwenye baadhi ya familia kila mara wanaumwa tumbo.

“Unaenda hospitali na kunywa dawa lakini baada ya siku kadhaa bado tatizo lile lile, kumbe chanzo ni maji wanayotumia kwa kunywa na kupikia hawajayapima ni machafu kwahiyo yanawadhuru,” alisema Wanjala.

Kwa sababu hiyo, …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles