Neema wanaotaka kuchukua mafao

0
2391

Na ANDREW MSECHU-DODOMA

WAFANYAKAZI wote wakiwamo wa umma na wasio wa umma ambao walikuwa wakiweka fedha zao kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii sasa wapewa uhuru kisheria wa kudai mafao yao muda wowote.

Hatua hiyo inatokana na wanufaika hao kuondolewa vikwazo vya muda wa kudai mafao yao, baada ya Bunge kupitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Namba Sita wa mwaka 2019.

Kwa maana hiyo, wanufaika hao watakuwa huru kudai mafao yao muda wowote wanaohitaji kufanya hivyo kulingana na utayari wao.

Muswada huo uliwasilishwa Bungeni na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi Septemba 12,mwaka huu ambapo wabunge waliridhia mabadiliko ya vifungu katika Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Hifadhi za Jamii Sura ya 135, iliyotungwa na Bunge mwaka 2008.

Akifafanua kuhusu mabadiliko hayo, Prof. Kilangi alisema …

Habari kamili jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here