23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kujenga hospitali ya kisasa Kibaha

Na MWANDISHI WETU

-KIBAHA

SERIKALI imeanza ujenzi wa hospitali mpya ya kisasa katika eneo la Kata ya Picha ya Ndege kwa lengo la kuwaondolea kero wananchi ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya.

Akizungumza jana na kuhusiana na ujenzi huo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Lulanzi  inapojengwa hospitali hiyo, Thobiasi Shilole , alisema    kukamilika   mradi huo kutaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa maeneo mbalimbali ya Kibaha.

Alisema hiyo ni kwa kuzingatia kuwa  awali walikuwa wanapata usumbufu mkubwa  wanapohitaji huduma ya matibabu.

  Mbunge wa Kibaha Mjini, Silvestry Koka (CCM),  ambaye alifanya ziara ya  kukagua ujenzi wa hospitali hiyo, alimpongeza Rais Dk. John Magufuli kwa kuamua kutoa   Sh bilioni 1.5 ya ujenzi huo.

Aliwataka wakandarasi kuhakikisha wanajenga majengo yenye ubora unaotakiwa  na kuachana na tabia ya kufanya kazi  ambazo zipo chini ya kiwango.

Koka alisema kutekelezwa kwa mradi huo   ni kutokana na juhudi ambazo alizifanya kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali  wa wilaya pamoja na serikali  kuu kwa ujumla.

Aliahidi kuendelea kuleta maendeleo kwa wananchi katika sekta mbalimbali.

“Huu mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya kwa kweli umeletwa kwetu kwa lengo la kuwasaidia wananchi katika suala zima la kuwasogezea huduma ya matibabu.

“Kwa hivyo ninatoa pongezi zangu za dhati   kwa Rais wa awamu ya tano, Dk. John Magufuli katika kuwaboreshea wananchi huduma ya afya pamoja na mambo mengine,” alisema Koka.

  Diwani wa Kata ya Picha ya Ndege,  Robert Machumbe (CCM), alisema serikali ya Awamu ya Tano inawaletea wananchi  mabadiliko chanya ya maendeleo katika nyanja mbalimbali.

Alisema  kwa sasa limepatikana  eneo la ekari 25 kwa ajili ya ujenzi  wa hospitali hiyo ya wilaya.

“Kwa kweli tunapenda kuishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuweza kutuletea mabadiliko chanya ya  maendeleo.

“Utaona kwa sasa katika kata hii ya picha ya ndege kuna hatua kubwa   ambayo tumeifanya katika nyanja mbalimbali na sasa tumeshaanza ujenzi wa hospitali yetu ya wilaya.

“Hospitali  itajengwa katika mtaa wa Lulanzi kwa hivyo hii ni hatua kubwa  pamoja na shule ya sekondari ambayo tayari eneo la  ekari 11.7 limekwisha kupatikana,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles