24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

RC Arusha awatahadharisha wazazi walioshindwa kuwahudumia watoto wao

MWANDISHI WETU-ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewaagiza wakuu wa wilaya zote za mkoa huo kukusanya takwimu za wazazi na walezi walioshindwa kutimiza wajibu wao wa kuwahudumia watoto wa wenye umri chini ya miaka 18 ikiwemo kuwasomesha.

Gambo ameyasema hayo leo kwenye kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa mkoa wa Arusha yaliongozwa na maandamano ya Jeshi la Polisi yaliyobeba kauli mbiu ya “Kizazi chenye usawa simama dhidi ya ubakaji.

 “Nitumie fursa hii kuwaagiza wakuu wote wa wilaya za mkoa wa Arusha wahakikishe  wanakusanya data zote za wazazi ambao wameshindwa kutimiza wajibu wao wa kuwasomesha au kuwahudumia  watoto wao ambao wako chini ya miaka 18.

“Lakini pia walete matukio ya ukatili  wa kijinsia yaliyoripotiwa kwenye wilaya zao ni hatua  gani zimechukuliwa mashauri mangapi yamepelekwa mahakamani, mangapi bado hayajapelekwa, sababu ni nini na kikwazo ni nani tutachukua taarifa zote na wazai waliojishau watimize wajibu wao wa msingi wa kuhudumia watoto wao,” amesema Gambo.

Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana, amesema wameshaanza kazi rasmi ya kuwadhibiti watu wanaofanya matendo ya ukatili wa kijinsia ikiwemo kuwachukulia hatua kali za kisheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles